Ray: Kama Huamini Sikulazimishi, Mi Maji Yananing’arisha!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

HIVI kari-buni gumzo kubwa mitaani pamoja na kwenye mitandao mingi ya kijamii ilikuwa juu ya staa wa Bongo Muvi, Vincent Kigosi ‘Ray’ baada ya kudai kuwa kunywa maji mengi kunamfanya aendelea kuwa mweupe.

Kauli hiyo alianza kuitoa katika mahojiano aliyofanyiwa katika Kipindi cha E-News kinachorushwa na EATV ambapo alisema kwamba huwa anakwenda saluni mara moja kwa wiki kwa ajili ya kusafisha uso wake (Scrub) pia na kunywa maji mengi.

“Zamani ilikuwa shida kuingia saluni kufanya scrub, sasa hivi najiweza katika hivyo vitu, kwa hiyo kwa kila wiki lazima nifanye scrub, nijitengeneze mwili wangu kama kioo cha jamii ninapotokea katika TV ili wewe Mtanzania uweze kuni-admire, kwa hiyo kimsingi sijichubui, nafanya sana mazoezi na kunywa maji mengi ndiyo siri ya ngozi yangu kunawiri,” alisema Ray.
Jamii kwa ujumla ilimchukulia tofauti na gumzo lililoenea kwenye mitandao ya kijamii ni pamoja na mashabiki wake wengi kufanya jaribio la kunywa maji mengi kwa mara moja huku wengine wakiunda makundi na kujiita Team Water Baby (TWB).

Showbiz Xtra ilifanikiwa kufanya mahojiano na Ray ambapo katika makala haya anafunguka yote;
Xtra: Kauli yako ya kufanya mazoezi na kunywa maji mengi, watu wengi wameichukulia tofauti, unazungumziaje hilo?

Ray: Siwezi kuwaongelea sana kwa sababu kila Mtanzania ana haki ya kuzungumza kile anachokiwaza kichwani kwake, kikubwa ninachoamini maji ndiyo yananifanya niwe na ngozi nyororo, basi! Kwa hiyo nafanya sana mazoezi na nikwambie tu hilo la kunywa maji mengi kama hawawezi basi siwezi kuwakataza ama kuwalazimisha kwangu inawezekana ndiyo maana naendelea kuwa mweupe. Hata kwenye familia yetu hakuna mtu mweusi na kama atatokea mweusi atabakia kuwa mweusi na kama mweupe atabakia kuwa mweupe.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Upuuzi mtupu kwani ukiwa mweupe ndo haufi?au utaenda peponi?africa bado sana wacha wazungu waendelee kutucheka.

    ReplyDelete
  2. Hakuna cha maji wala upuuzi wa maji, huyu mtoto anakula mkorogo kama kawaida ya wanaojichubua. Kama ni maji basi anayatumia kunywea vidonge vya kujichubua kama wazaire wanavyosema.. Asituletee ujinga wake wa kutaka kuwa mweupe kama mzungu.. apeleke ujinga wake huko kwa wabongo movi wenzie

    ReplyDelete
  3. DaRay bado maboobs na makalio saiv hujatia mana tayar mweupe ushanyowa nyusi na ushatia nywele kali.

    ReplyDelete
  4. Ili wachumba waje walete posa kwenu.

    ReplyDelete
  5. kubwa zima hovyo we ngozi yako tunaijua ni nyeusi we ulikuwa kama baracka da prince
    leo uko kama marehem michael jackson
    ebu kasome vizuri faida za maji kwa ngozi
    tatizo elimu sijui me bongo movie imeishia kula mkorogo

    ReplyDelete
  6. mkoroooooooooooooooooooooooooooooooogo. demu wake ana moyo maana wanashare vipodozi.

    ReplyDelete
  7. Ok ungenyamaza bora au kufikiria movie nyengine hizo nyusi na wanja

    ReplyDelete
  8. kama hamtaki si basi ... na nyinyi jaribuni kujua ukweli

    ReplyDelete

Top Post Ad