Wingu Zito Laendelea Kutawala Ufisadi Wa Mabilioni NIDA....Yadaiwa Kitambulisho Kimoja Kimegharimu Sh 89,800

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wingu  zito limetanda ndani ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kuhusu matumizi ya  Sh bilioni 179.6 ambako kila kitambulisho  cha taifa kimegharimu Sh 89,800 zikiwamo gharama za utawala

Hayo yamebainika  siku chache baada ya Rais Dk. John Magufuli kushangazwa na watendaji wa mamlaka hiyo ikizingatiwa vitambulisho vilivyokwisha kutengenezwa hadi sasa havifiki   milioni mbili na havina saini.

“Utaona ugumu wa kuongoza, nchi inatawaliwa na madudu ya kila aina.  Wapo watu wanacheza na fedha wanavyotaka wakati wapo watu masikini sana  wengine wanataka bodi zao wakakae Ulaya.

“Hapo ndipo tulipofikia, wengine wanalipwa mshahara wa Sh milioni 35 kwa mwezi…naomba mniombee kabla ya kunihukumu, toeni hukumu kwa haki kwa hawa wanaotaka kuifikisha nchi pabaya, toeni hukumu zao haraka,” alisema.

Rais Dk. Magufuli, licha ya kushangazwa na hali hiyo, alisema Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ilipewa Sh bilioni 70 lakini iliweza kutengeneza vitambulisho   23,253,982 ambavyo vilikuwa na saini ya kila mpiga kura na kila kimoja kimegharimu Sh 3,010.

Kutokana na hali hiyo, tofauti ya gharama kati ya kitambulisho kimoja cha NIDA na cha NEC ni Sh 86,790.

Pamoja na hayo, hivi sasa Watanzania wanasuburi   ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Juma Assad, kuhusu  matumizi ya fedha hizo za NIDA.

Januari 26 mwaka huu, Rais Magufuli alitangaza kumsimamisha kazi ili kupisha uchunguzi dhidi yake, Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dickson Maimu.

Maimu alisimamishwa kazi pamoja na maofisa wengine wanne, kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za Serikali.

Maofisa hao ni Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Joseph Makani, Ofisa Ugavi Mkuu, Rahel Mapande, Mkurugenzi wa Sheria, Sabrina Nyoni na Ofisa Usafirishaji, George Ntalima.

Akitangaza uamuzi huo, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Sefue, alisema taarifa zilizomfikia Rais zinaonyesha kuwa NIDA hadi wakati huo ilikuwa imetumia Sh bilioni 179.6, kiasi ambacho ni kikubwa.

Alisema Rais angependa ufanyike uchunguzi na ukaguzi kujua jinsi fedha hizo zilivyotumika, maana amekuwa akipokea malalamiko ya wananchi kuhusiana na kasi ndogo ya utoaji wa Vitambulisho vya Taifa.

Licha ya kumuelekeza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, afanye ukaguzi maalumu wa hesabu za NIDA  ukiwamo ukaguzi wa “value for money” baada ya kuthibitisha idadi halisi ya vitambulisho vilivyotolewa hadi sasa, pia aliitaka Takukuru ifanye uchunguzi kujiridhisha kama kulikuwa na vitendo vya rushwa au la.

Credit: Mtanzania
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Na hapa napo tunasubiri uchunguzi wa nini?

    ReplyDelete
    Replies
    1. apo chacha rais akisema wanasema anakurupuka

      Delete
    2. JPM akisema ,Mara ooo, kaingilia katiba kwa madudu haya Ata aitwe dicteta , Mr president tumbua wao mpaka wanyooke , mbwembwe za mm nafanyia bandari, cijui TRA, Mara Nhc, mtaelewa Tu huu mwaka

      Delete
  2. Amri itoke Msoga

    ReplyDelete
  3. Msoga inahusiana nini hapo mkuu? Ama unamaanisha mzigo mwingine wa NIDA umefungiwa msoga?

    ReplyDelete
  4. Bongo hiyo kila mkuu anamiliki gorofa Na magari makubwa walinzi kila Kona wanyonge foleni ndefu jua kali tunasubiri vitambulusho Na kupigwa picha Go Go Mr President tulikuchagua wenyewe

    ReplyDelete

Top Post Ad