Dudubaya Afunguka...Watu Mfano wa Chid Benz Hawatakiwi Kusaidiwa Kabisa...Kifo Anakitaka Mwenyewe

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Baada ya rapa Chidi Benz kuomba msaada ili asaidiwe kuirudisha afya yake ambayo imethorofika kutokana na matumizi ya Madawa ya kulevyana na baadae kusaidiwa na Babu Tale kwa kupelekwa rehab. Wadau mbalimbali pamoja na wasanii wenzake walimpongeza Babutale lakini Dudu Baya amedai hakupenda rapa huyo asaidiwe.
Dudu

Akizungumza na Bongo5 Jumamosi hii, Dudu amedai rapa huyo hakuwa tayari kusaidiwa ndio maana baada ya kusaidiwa anataka kujipangia baadhi ya mambo.

“Watu mfano wa Chidi Benz hawatakiwi kusaidiwa, niwakuachwa wafe na wazikwe. Kwanza ni waongo, ukikutana nao utasikia naumwa au nimefiwa, utampa msaada, mwisho wa siku anaenda kujidunga. Misaada kama hii inatufanya majina yetu kuwekwa kataka orodha ya wauaji (killers),” alisema Dudu.

Aliongeza, “Babutale na wenzake walipomfisha Chidi Benz rehab kwanza alianza kuweka masharti yake kituoni, mara hawezi kushauriwa na mtu ambaye hajawahi kutumia sumu hiyo (unga). Hapo ndipo nilipogundua amebebwa kinguvu bila yeye kuwa tayari kupona. Ni sawa na mgonjwa apelekwe hospitali then aanze kutoa masharti yake, eti hiki kitanda sikitaki. Wewe dokta huwezi kunitibu kwa sababu hujawahi kuumwa ugonjwa ninaoumwa, mgonjwa kama huyo si nachotaka ni kifo?. Hata wakati yesu amekuja kutukomboa na dhambi, aliponya wagonjwa waliokuwa tayari kupona, hata leo umpeleke ndugu yako kanisani au msikitini akaombewe aache ulevi au umalaya, kama hana dhamira ndani ya moyo wake ya kuacha, hakiwezi tokea chochote,”

Pia Dudu amesema wasanii wengi wanasikia kila siku kuhusu madhara ya Madawa ya kulevya lakini wanapuuzia.

“Chidi Benz si mtoto mdogo, ameshuhudia wasanii na watu wa kawaida wengi tukiwapoteza kwa sababu ya Madawa ya kulevya lakini wanapuumzia, wanarudia kubwia tena. iweje leo yeye ajiingize kataka ulimwengu huo? hakika kifo anakitaka mwenyewe na si kurubuniwa. Uzuri wa Tanzania hatuna umasikini wa ardhi, watu kama hawa hawana faida kwa taifa, niwakuacha wafe na wazikwe. Na kama inawezekana Mh Rais Magufuli angetoa amri mateja wakifa wazikwe na jiji. Kwa sababu sioni ndugu yeyote wa Chidi yuko bize na rapper huyo. Kwanini nyingi mumpaparikie au ndio mnauchukungu kuliko ndugu zake?. Asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu,” alisema Dudu.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hujafa hujaumbika. Ulevi wa unga, pombe,niugonjwa mwingine kama kisukari au kansa. Usilete ubisha usiokuwa na faida. Ninacho kisema ninauwakika nacho, ua nikwambie kuwa mimi ni msomi mzuri. Dudu baya elimuyako iko namna gani, umesoma au la.
    Mungu ibariki Afrika.
    JB.

    ReplyDelete
  2. Asante dudu umeongea ukweli mchungu...lkn Muombe Mola kila leo akuepushe na majaribu ya dunia sie sote binadamu mitihan tumeumbiwa...huu ni mtihani kwa chid na nijaribu lake Mungu amsamehee amsaidie apone nahakika keshajifunza...kilichobaki tusimseme sana tumpe sapoti keshakosea nayy si malaika asikosee

    ReplyDelete
  3. Huyu dudu baya kashaanza fujo kwa nini asisaidiwe kama uwezo upo kosa si kosa kurudia kosa ndio kosa elimika kidogo

    ReplyDelete
  4. The dudus,ngumi jiwe

    ReplyDelete
  5. Ni kweli naungana Na dudu baya sema babu tale anatafuta ulaji hapo kwa wahisani

    ReplyDelete
  6. Hizo speech zako pekee zinaonesha nawe pia unatakiwa kufuata chidi rehabilitation

    ReplyDelete

Top Post Ad