Mr Nice Afunguka Kuhusu Picha yake Akiwa Amekonda Iliyoshtua Watu...Adai Alilishwa Sumu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

SIKU chache baada ya kusambaa kwa picha yake inayomuonesha akiwa amepungua mwili na kuzua mjadala mitandaoni huku wengi wakimuonea huruma, mkongwe wa Muziki wa Takeu, Lucas Mkenda ‘Mr. Nice’ ameibuka na kufungukia afya yake.

Picha inayomuonesha Nice akiwa amepungua mwili ilizagaa mapema wiki hii kwenye mitandao ya kijamii ambapo wengi waliochangia mjadala wa picha hiyo, walisema staa huyo aliyetikisa kwa utajiri enzi hizo, kwa sasa atakuwa anaumwa sana huku mjadala mkubwa ukawa ni ya lini?

Baada ya Ijumaa kuinasa picha hiyo, lilifanya jitihada za kumpata msanii huyo kwa kumvutia waya alipopatikana, alifunguka kwa kirefu kuhusu afya yake:

“Kwanza hiyo picha ni ya kitambo sana. Si unakumbua lile sakata langu la mimi kulishwa sumu kwenye chakula? Basi ndiyo kipindi kile.

“Namshukuru Mungu niliiwahi ile sumu na kupewa dawa ambazo natumia mpaka sasa. Kweli nilipungua lakini ni wakati huo, kwa sasa sipo hivyo kama kwenye hiyo picha inayosambazwa mitandaoni,” alisema Mr. Nice.

Akaongeza kuwa ni kweli afya yake haiko poa sana kwa kuwa bado anaendelea kutumia dawa za kuimaliza sumu ile lakini siyo kama vile anavyoonekana kwenye picha hiyo.

Chanzo: GPL
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mgeni keshamtembelea huyooo sumu gani unywe dawa miaka yote hii..na hizo sumu mnalishwa mkiwa wapi waache kulishwa wakina obama na trump mlishwe nyie...maana sasa kila msanii utasikia nimelishwa sumu

    ReplyDelete
  2. Dah ebwanaa pole sana Anza ibada haraka sana mungu atakusaidia na hiyo picha ungeiondoa

    ReplyDelete
  3. MAISHA DAAAH, KWELI MZUNGUKO MAMAAEEE

    ReplyDelete
  4. Eti kalishwa sumu!!!

    ReplyDelete

Top Post Ad