Uchambuzi wa Humphrey Polepole Kuhusu Marekani Kusitisha Msaada wa Mabilioni ya Pesa na Shughuli zake Tanzania

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Nianze na nukuu hizi mbili kuntu za Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere- Mwenyezi Mungu amrehemu.


“Democracy is not a bottle of Coca-Cola which you can import. Democracy should develop according to that particular country”. June 1991 in Rio De Janeiro, Brazil

"Demokrasia sio chupa ya Coca-Cola ambayo unaweza kuagiza. Demokrasia lazima ikue na kuendelezwa kulingana na nchi husika". Juni 1991 Rio De Janeiro, Brazil (Tafsiri ni yangu)

“No nation has the right to make decisions for another nation; no people for another people”. From ‘A Peaceful New Year’ speech, Tanzania, January 1968

"Hakuna Taifa lina haki ya kufanya maamuzi juu ya Taifa lingine; wala watu juu ya watu wengine ". Hotuba ya Amani ya Mwaka Mpya, Tanzania, Januari 1968 (Tafsiri ni yangu)

Hili la Marekani na uamuzi wa MCC ni jambo la mpito na haliwezi kuua mahusiano yetu na Marekani. Tanzania na Marekani zinashirikiana kwa mambo mengi na MCC ni sehemu tu tena ni eneo jipya la ushirikiano.

Uamuzi huu ni jaribio kwa uhuru wa Taifa letu. Hakuna namna nyingine ila kushinda hili kama tulivyoshinda mengine huko nyuma. Kwa wale ambao wameuona umri watakumbuka namna tulivunja uhusiano na Ujerumani Magharibi 1964 pale walipotaka kuwa na kauli hasi dhidi ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Tulivunja uhusiano na Ujerumani Magharibi baada ya kutaka kuingilia Uhuru wa Mataifa Mawili huru yaliyoamua kuungana na kuunda Nchi Mpya ambayo leo tunajivunia, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

1965 Tulivunja uhusiano na Uingereza kufuatia na kitendo cha wazungu wachache kujitangazia Uhuru (Unilateral Declaration of Independence) kule Rhodesia na uingereza kukaa kimya na kushindwa kuchukua hatua stahiki.

Tulivunja Uhusiano na Uingereza kuieleza Dunia kwamba Uhuru wa nchi za Afrika ni kipaumbele muhimu kwa Tanzania. Jambo tunalopaswa kufahamu ni kuwa MCC 2 toka mwanzo imekuwa ni mtihani dhidi ya uhuru wetu.

Napenda ieleweke kwamba kipindi hiki kilichotokea sio kuvunjika kwa uhusiano wetu na Marekani bali taasisi ya MCC ndio imesitisha msaada wao kwetu, lakini mahusiano yetu na marekani bado yako pale pale, na si Marekani au Tanzania inayoweza kuugharimu uhusiano wetu.

MCC 1 ilikuwa ni chambo cha kutuvuta na tulipewa bila masharti tena hela nyingi dola milioni 698 na ni fedha tulizopewa moja kwa moja na kupewa uhuru wa kuamua tuzitumieje.

Tanzania ilitakiwa kuainisha maeneo kisha wao wanatoa hela. Ndio maana miradi kama ile barabara ambazo hazikuwa zikipata ufadhili kwa kuwa hazikuonekana ni za kiuchumi na miradi ya maji ya Morogoro na kwingineko iliingizwa humu na kupata ufadhili.

MCC 2 sio hivyo. Kwenye MCC 2 walengwa wakubwa ni sekta binafsi ya Marekani, hapa kuna mtego hapa, hapa ni biashara hapa.

Mchakato wa MCC 2 ulipoanzishwa, wafanyabiashara kwa kushirikiana na Maseneta wakaanzisha hoja kuwa kwanini Marekani inatoa fedha kwa ufadhili katika nchi ambazo China ndio wenye kufaidika na fedha hizo?

Wakaleta hoja ya kuwa Serikali ya Marekani ifanye jitihada ya kuweka fedha kwa kusaidia Sekta Binafsi ya Marekani kupenya Afrika.

Ukaitishwa mkutano wa US-Africa Summit na agenda kubwa ikawa Power Africa. Katika Power Africa, Marekani ikalichagua eneo la Nishati (si uzalishaji viwanda) kwa kutambua kuwa ndio eneo pekee wanaloweza kushindana na wachina.

Wakasema wataelekeza fedha huko kuisaidia Afrika kutatua tatizo la nishati ambalo ndio pembejeo ya viwanda. Wakaweka sharti kuwa fedha hizo na miradi hiyo itatekelezwa na Sekta Binafsi ya Marekani.

Ndio sababu wengi wenu mtakumbuka hata Rais Obama alitangazia dhamira ile pale Ubungo kwenye Mitambo ya Symbion Power na sio kwamba alipenda kwenda kutembea Ubungo.

Kuanzia hapo kumekuwepo na shinikizo kubwa sana na masharti magumu na yenye kuhamahama (shifting goal post) kutaka kuibaka sekta ya nishati nchini ikiwemo mageuzi ya TANESCO.

Zikaainishwa hatua kadhaa,ambazo utekelezaji wake baadhi ni kisheria na kisera na hivyo haziwezi kwenda kwa deadline walizotaka.

Kila bodi ikikutana wanaibua hiki na kile lakini wakisema hela watatoa. Hela hizi zikawa zimeshikiliwa kama chambo ukisogelea zinasogea, ni sawa na ule mchoro wa Mpanda Punde aliyeshika fimbo yenye majani na akiielekeza mbele ya punda, kwamba punda ataendelea kuyafuata majani akidhani atayafikia kumbe ndio anaupiga mwendo.

Hatimaye wakasema wanasubiri uchaguzi mkuu jambo ambalo halihusiani na madai ya mwanzoni. Baada ya uchaguzi wakaibuka na suala la Zanzibar.

Hivyo, uamuzi wao wa leo ni uamuzi uliotarajiwa. Pia ni uamuzi wenye madhara kwa sekta binafsi ya Marekani pia ambayo ndio ilikuwa itekeleze miradi hiyo.

Kama Taifa ni muhimu kulinda utu na uhuru wetu. Ndio msingi wa sera yetu ya nje toka mwanzo na hata sasa. Tumetofautiana na Marekani katika hili tutapatana katika mengine. Ndio uhai wa maisha ya diplomasia.

Wao nao wanayo hadhira ya wapiga kura wao wanayojaribu kuituliza huko nchini kwao kwa uamuzi huu. Tunapaswa kuheshimu uamuzi wao kama ambavyo wanapaswa kuuheshimu wetu.

Hatimaye baadae tutapatana. Marekani inaihitaji Tanzania zaidi na Tanzania inaihitaji Marekani. Marekani inahitaji MCC 2 zaidi hali kadhalika Tanzania inahitaji MCC 2.

Mahusiano ya Tanzania na Marekani hayakuanza na hayataisha na MCC. MCC imeyakuta na itayaacha.

Kama marudio ya uchaguzi wa Zanzibar ndio kigezo, basi Marekani isingekuwa inatoa zaidi ya Dola Bilioni 3 kila mwaka kwa Egypt iliyo chini ya utawala wa kijeshi kwa sababu ya kuununua ugomvi wa Egypt na Israel na isingetoa kiasi cha dola bilioni 6 kwa Israel kila mwaka kwa yale wanayoyafanya dhidi ya Wapalestina.

Huu ni wakati ambao Taifa linawaita Wazalendo wake. Wazalendo wasimame na kusema 'Nchi yangu KWANZA, iwe Sahihi au Imekosea" na Makuwadi watashangilia na kusema "si mnaona sasa kiko wapi?".

Huu ni wakati wa kujifunga mikanda na kulinda heshima yetu kama Taifa letu. Tuna vyanzo vya mapato vingi sana ambavyo hatujaanza kukusanya mapato, tuwe wabunifu na tusibweteke na kutegemea mapato yataongezeka maradufu kwa vyanzo vile vile.

Niseme kwa uchache, sababu walizotoa MCC, na ieleweke aliyetoa tamko ni MCC, heri lingetoka tamko hili Wizara ya Mambo ya Nje au Ikulu ya Marekani, moja ni Zanzibar na pili ni Sheria ya Makosa ya Mitandao (Cyber crimes Act).

Sasa hebu tujadili kidogo, hivi kule Zanzibar tulitaka kitokee nini pale ambapo wanasiasa walikuwa hawataki kujadiliana?

Tume ile ile ya Uchaguzi ambayo bado ilikuwa na uhalali wa kikatiba na kisheria kuuitisha, kuufuta na kuuitisha tena uchaguzi ikachukua nafasi yake.

Wanasiasa wasio makini wakaishia kuhamishia malumbano mitandaoni badala ya kuitafuta suluhu ya kisiasa na pale siasa iliposhindikana basi wangeitafuta suluhu katika mahakama za Zanzibar.

Mezani wakashindwa, mahakamani hawakwenda. Tume ikachukua uongozi, uchaguzi ukaitishwa Wananchi wakapiga kura na sasa huko Zanzibar kuna serikali na baraza la wawakilishi.

Hata mimi sifurahii sana njia waliyoichukua Zanzibar lakini ilibidi siasa za madaraka zisite ili tuanze kufanya siasa za maendeleo. Je wamarekani walitaka muujiza gani utokee huko.?

Kuhusu Sheria ya Mitandao, hata mimi siipendi, si twende mahakamani, bunge litaanza vikao muda si mrefu je wabunge si wapeleke hoja ya kuifanyia marekebisho sheria hii.

Sasa Marekani (MCC) inapoweka shinikizo kwa suala la Sheria ambayo ni jambo la ndani na linaloweza kujadilika, sijaelewa.

Mbona sie hatujapiga kelele Yule jamaa yao Trump alipotutusi waafrika na kusema sisi stahili yetu ni kuwekwa tena chini ya ukoloni (hapa nimechomekea tu).

INDHARI

Ni aibu kwa viongozi wa kisiasa kufurahia jambo hili, ni ishara ya ukuwadi wa kisiasa na ambao uko tayari kukumbatia mahusiano yanayotweza Uhuru wetu. It is now high time kufanya siasa safi za maendeleo (politics of development) na sio kujikita katika katika siasa za madaraka (Politics of Power).
*************

Imeandikwa  na: Humphrey Polepole.
Mwandishi, Ndg. Humphrey Polepole amenufaika na uelewa wa watu wenye uzoefu wa mahusiano ya Tanzania na nchi za Nje. Aidha, ni mnufaikaji (alumni) wa programu ya uongozi chini ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

16 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Marekani na nchi za ulaya azilazimishi chochote hapa tanzania wa isipokuwa tanzania kama nchi ilita wakaguzi kusimamia uchaguzi na wasimamie wote waliokuja wamesema uchaguzi wa kwanza haukua na dosari,sasa ccm mnafikiri demokrasia ni kufanya mtakanyo hata kama iwe kuvunja sheria eti marekani wanauhusiano wa siku nyingi na tanzania wewe unafikiri marekani walikuwa hawana uhusiano na Zimbabwe,libya, nigeria,irak,sudan,nk subiri utafurahi wakati mbuzi analamba reli

    ReplyDelete
    Replies
    1. wewe utakuwa wapi au ndio utashinda mitandaoni kila kukicha bila kufanya kazi,aibu yako.Hapo ulipo hata senti mfukoni huna bado unashabikia nchi kunyimwa misaada,yaani hiki kizazi cha nyoka kimelaaniwa hata bwana Yesu amesema.

      Delete
  2. In fact we can do without the American money if it requires us to bend,
    Neither america nor any other country on earth have the right to interfere with our political processes any how
    Just ask Magufuli to go to Beijing and we will be sorted look at Zimbabwe they never accept bending to them for nearl 15 years now cos America and its west allies will next ask for Tanzania to have GAY ministers.

    ReplyDelete
  3. Polepole ni mmoja ya watu aliowaita mkapa kuwa ni malofa.. kwanini ccm wanasema hii ni nchi ya kidemocrasia wakati wanaiogopa? Mkitaka kujuwa polepole ni lofa mmeona hata JPM hajamfikiria na kumpa nafasi yoyote

    ReplyDelete
  4. pole sana polepole! uelewi kitu!

    ReplyDelete
  5. Tatizo nchi zetu hatuna demokrasia Mr Pole ole,wewe endelea kufikiria pole pole na akili zako za pole pole.

    ReplyDelete
  6. Hongera kwako unae elewa

    ReplyDelete
  7. Wanaiba matirion katika bara hili, alafu kerere nyingi na vimisaada vyao mbuzi peleka huko matako yao, michosho sana hawa watu, wanajifanya misaada misaada, na yale marition wanayotuibia, tena wanawadanganya na hawa viongozi wetu mangungo wasiojielea, kwa tuhela tudo tudogo tu, wenyewe wanaishi vizuri sisi huku tunateseka kwa tumissada twao mbuzi na mashriti kibao,

    ReplyDelete
    Replies
    1. UMENENA ANONY 9.38 AM, TUKIENDEKEZA MISAADA YAO AMBAYO HAINA KICHWA WALA MIGUU TUTAISHIA KUWA NA NDOA ZA JINSIA MOJA KAMA MOJA YA MASHARTI TULIYOPEWA NA BADO HATA WANAWAKE WATAAMBIWA KUSAGANA NI DEMOKRASIA KAMA ILIVYOKUWA KWA WANAUME, KWA HIYO USHABIKI WETU UTATUWEKA PABAYA KWA KUSHABIKIA VITU AMBAVYO SIYO UTAMADUNI WETU

      Delete
    2. Tena Anon na hizo ndoa za jinsia mmja, zikishika hatamu. na kuwani sehemu mmja ya utamaduni,tutakuja kuchekwa na kubezwa zaidi.sisi watu weusi ni wa ajabu sanaa tutambiwa ni wajinga, tena watafikia hatua ya kutuita wanyama, kwa kuwa watasema binadam wa kawaida hawezi kufanya hivi, haya mambo ya kiayawani,hawa hawa wanaowashinikiza hizo ndoa. Wazungu, wanapenda kumuona mwafrika anangaika na umasikini ili wao wapate njia ya kujichotea, wewe unafikiri wanaume wengi wakiwa katika khali hiyo ni Taifa au bara tena ni hatari, nguvu kazi yote kwinshinei, kila dume litakuwa jike, haya nguvu kazi iko wapi tena?, mungu alivyoumba anajua mwenywe, ndio maana akaweka mume, mke, hawa hawa wazungu kwenye mataifa yao. hawapendi eti wanaume kuwa hivyo, tena hawapendi kweli kweli, jamiii unaona inasema chini chini tu, tena wanakwambia, yote hii ni kutokana na mtu furani alikuwa hivyo na alipopata mwanya wa siasa akatumia huwo mwanya, ili na wengi wasiogope, kuna familia zingine baba kajitoa kabisa na kamkimbia mama kwa kuendekeza mtoto wake na haya mambo. baba hataki hata kujiusisha na chochote, anasema wamuache na maisha yake, ni wazungu hao

      Delete
  8. HALAMBWI MTU MIGUU HAPA Hata wao wanamasikini kwao wakawasaidie ndugu zao kwanza wanakuja kwa jina la misaada kuiba rasilimali zetu wakafie mbali

    ReplyDelete
  9. HALAMBWI MTU MIGUU HAPA Hata wao wanamasikini kwao wakawasaidie ndugu zao kwanza wanakuja kwa jina la misaada kuiba rasilimali zetu wakafie mbali

    ReplyDelete
  10. Hakuna kubabaika na america hii ni nchi huru hatubabaishwi na misaada suala la kukatiwa misaada halijaanza jana. Anayetaka kutusaidia karibu ila si kwa maahart. Kwan bush alivyopora uahondi wa algore nan aliwazomea america?watanzania tuachane na wanasiasa vibaraka kwa kuwa wanabembeleza visa. Hapa uzalendo bravo sana pole pole

    ReplyDelete
  11. Uzalendo kwanza, Tanzania kwanza...Marekani ndio nani

    ReplyDelete
  12. Kila serikali duniani ina wanaoiunga mkono kwa maamuzi yake hivyo hatushangai kuona mkitetea serikali ya ccm sasa tusubir kama nchi hii inayotegemea kila kitu kutoka nchi za nje kuanza akubeba gunia la pesa kwenda kununua mate 65% ya bajeti ya nchi ni misaada leo tunaleta ujeuri

    ReplyDelete

Top Post Ad