Atupwa Jela Miaka Saba Baada ya Kujerui Watu Wawili Kwa Kutumia Wembe..

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 Mahakama ya Wilaya ya Ilala, imemhukumu kifungo cha miaka saba jela fundi umeme, Lipyana Ndumbaro (29) baada ya kupatikana na hatia ya kujeruhi kwa kutumia wembe.

Mahakama pia imemtaka Ndumbaro kumlipa fidia ya Sh2 milioni mlalamikaji.

Ndumbaro ambaye ni mkazi wa Mvuti wilayani Ilala, hakuwapo mahakamani hapo wakati hukumu hiyo inatolewa baada ya kuruka dhamana.

Akisoma hukumu hiyo jana, Hakimu Mkazi, John Msafiri alisema Mahakama imemtia hatiani mshtakiwa huyo baada ya kuridhika na ushahidi wa mashahidi saba uliotolewa mahakamani hapo.

Hakimu Msafiri alisema Mahakama ilipokea vielelezo vitatu ambavyo ni picha, maelezo ya mgonjwa na fomu namba tatu ya Polisi (PF3).

“Kupitia ushahidi huu, Mahakama imeridhika na ushahidi wa upande wa mashtaka uliotolewa mahakamani hapa bila kuacha shaka,” alisema Hakimu Msafiri.

Kabla ya kutolewa kwa adhabu, Wakili wa Serikali, Neema Moshi aliiomba Mahakama kutoa adhabu kali ili liwe fundisho kwa watu wengine wanaofanya vitendo kama hivyo.

Katika hati ya mashtaka, ilidaiwa mshtakiwa alitenda matukio hayo kwa watu wawili tofauti.

Ilidaiwa Machi 17, 2014 maeneo ya Mvuti wilayani Ilala, alimkata kwa wembe Watunde Abdallah sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsababishia maumivu.

Pia, tarehe na mwaka huohuo, alimkata kwa wembe Shaban Kivanga na kumsababishia maumivu.  

Soma Nafasi za Ajira Hapa: www.ajirayako.com 


----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad