Breaking News: Mbunge Saed Kubenea Apatikana na Hatia Mahakani...Amehukumiwa Kifungo Hichi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemtia hatiani Mbunge wa Jimbo la Ubungo Saed Kubenea kwa kosa la kutoa lugha chafu ya matusi kwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Mbunge huyo amehukumiwa kifungo cha miezi mitatu nje kwa masharti ya kutorudia kosa la namna hiyo katika kipindi hicho na endapo atarudia kosa hilo basi atakuwa amevunja masharti ya kifungo hicho na kustahili kifungo cha gerezani.

Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba amesema baada ya kupitia ushahidi na vielelezo vilivyotolewa mahakamani hapo mtuhumiwa amepatikana na hatia baada ya upande wa mashtaka kuthibitisha bila chembe ya wasiwasi kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo.

Hukumu hiyo imefuatia ushahidi uliotolewa na mashahidi watatu kwa upande wa mashtaka wakiongozwa na Mheshimiwa Makonda huku upande wa utetezi ukiwa na mashahidi watatu akiwemo Kubenea mwenyewe.

Saed Kubenea alikuwa anakabiliwa na shtaka la kutoa lugha chafu kwa Makonda wakati wakiwa katika Kiwanda cha Ushonaji na Usafirishaji wa nguo cha Tooku Garments Co. Ltd kilichopo maeneo ya Mabibo External baada ya kutokea kutokuelewana baina ya viongozi hao walipokwenda kutatua mgogoro wa wafanyakazi wa kiwanda hicho na wamiliki.

Katika kesi hiyo, Kubenea anadaiwa kumtolea lugha chafu Makonda kuwa ‘wewe kibaka, mpumbavu, mjinga na cheo chenyewe cha kupewa tu’.

Upande wa mashtaka ulikiri kutokuwa na rekodi yoyote mbaya ya mtuhumiwa huyo na kwamba hili ni kosa lake la kwanza lakini wakaiomba mahakama itoe adhabu kali ili iwe fundisho kwa watu wengine.

Awali, akijitetea baada ya kutiwa hatiani Kubenea alisema, hakwenda pale kwa nia mbaya ya kutukana bali alikwenda kutatua mgogoro uliokuwepo baina ya wafanyakazi na wamiliki wa kiwanda hicho na kwamba hakuwa na miadi yoyote na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda ya kukutana pale.

Akijitetea zaidi Kubenea aliiomba mahakama impatie adhabu nafuu kwakuwa yeye ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo ameajiriwa kuwatumikia wananchi.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad