Dogo Aslay Kaongea Kwanini Hayuko Tena na Mwanamke Aliyekua na Ujauzito Wake… Umeneja Mpya Je?

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Aslay ni mwimbaji kutokea kundi la Yamoto BAND, kilichofanya awepo kwenye hii post ni kauli yake ya kukanusha kumtelekeza Mwanamke mwenye ujauzito wake baada ya kuishi nae kwa miezi isiyozidi 6.

Aslay ambaye ana umri wa miaka 20 sasa hivi amesema ‘Baada ya kuishi pamoja miezi sita tulizinguana ikabidi kila mtu ashike hamsini zake, sisi vijana bwana mambo mengi… tukaangalia pia mimi bado umri wa kukaa na Mwanamke na yeye akaona bado umri wake wa kukaa na Mwanaume‘


‘Sikuchukua uamuzi ila wote ndio tulichukua uamuzi…. nilimuacha na ujauzito wangu na tayari amejifungua mtoto wa kike ambaye ana kama mwezi mmoja na nusu, mwanangu nimemuita Moza jina la marehemu mama yangu… na bado mpaka sasa tunaonana hata hapa nimetoka kumuona mwanangu, hatujarudiana…. tunashirikiana tu kama mtu na mzazi mwenzake‘ – Aslay

Kingine alichokiongea Aslay kwa sasa ni kwamba amekabidhiwa majukumu mapya ya kuwa meneja, aliyemkabidhi ni boss wake Mkubwa Fela kiongozi wa Mkubwa na Wanawe na sasa Aslay ni meneja wa madada watano aliokabidhiwa miezi mitatu iliyopita na watasikika very soon.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad