AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA
Akizungumza jana na waandishi wa habari Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mohamed Mchengerwa ambaye pia ni Mbunge wa Rufiji alisema hatua hiyo imefikiwa baada ya kamati hiyo kufanya ukaguzi katika jengo hilo na kubaini limejengwa chini ya kiwango.
“Tumetembelea jengo hilo na kujionea limetumia fedha nyingi lakini limejengwa chini ya kiwango kwani halina hata miaka tisa lakini lina ufa mkubwa ambao unahatarisha maisha ya wafanyakazi ndani ya jengo hilo,” alisema Mchengerwa.
Alisema jengo hilo limetumia zaidi ya Sh bilioni 8 katika ujenzi, lakini limejengwa chini ya kiwango.
Aliongeza kuwa kisheria fedha zilizopangwa kwa ajili ya mradi huo zilitakiwa zibaki asilimia 20 kwa ajili ya ukarabati lakini zimebaki Sh milioni 200 tu na hakuna maelezo ya kujitosheleza.
Mchengerwa alisema hali hiyo imesababisha kamati hiyo kuagiza uchunguzi ufanyike na wataalamu waliohusika wachukuliwe hatua za kisheria kwa kufunguliwa kesi za jinai na madai.
Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu
Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:
NAFASI ZA AJIRA
JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA
GOODLUCK