Mzee Yusuph Aamua Kufunguka Kuhusu Wake Zake...Adai Wanamuumiza Kichwa Sana Kiasi cha Kumvuruga Akili

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mkurugenzi wa Kundi la Jahazi Modern Taarabu, Mzee Yussuf amesema hakuna kitu kinamuumiza kichwa kama kutoelewana kwa wake zake wawili.
mzee2

Akizungumza katika kipindi cha Sporah Show cha Clouds TV, Mzee Yussuf amesema anapitia wakati mgumu sana kuwamiliki wake wawili anaowapenda wakati wao hawapendani.

“Kusema kweli napata wakati mgumu kuwahandle, yanii linanivuruga sana hili swala,” alisema Mzee Yussuf. “Ndio maana natamani hata kesho waelewane. Sometime ni raha wakiwa hawaelewani kwa maana hata kama nimeenda pahali labda nimezunguka hakuna anayelinda” alifafanua zaidi.

“Lakini hii ni chugu sana, hili kwangu ni tatizo, natakamani leo au kesho waelewane. Lakini tatizo la hawa yote ni watu wa karibu, ndio maana mimi nimeshawaambia kwa mdomo wangu, hili jambo nataka liishe, sitaki kusema naomba liishe kwa sababu nilishawaomba sana, na ninachoona ustaa ndio unawasumbua wanashindwa kujua mimi ni staa zaidi yao,” aliongeza Mzee Yussuf.

Mwanzo wa mwaka huu, Mzee Yussuf alidai wake zake Leila Rashid na Chiku awamekatazwa kutumia mtandao wa Instagram kwa madai mtandao huo unakuza ugomvi wao.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. mbona na Leila Rashid ni msanii mkubwa tu sio wewe peke yako mzee Yusufu, ila wanaume kwa kujisifia wenyewe mpaka basi kwani ulitegemea nini kuoa wake wawili lazima wivu utakuwepo tu

    ReplyDelete
  2. Leila bonge la mwanamke,bonge la msanii,ana nyota ya kupendwa na mashabiki,anacheka na kila mtu,binafsi huwa naenda taarabu kwa kumfuata Leila tu.

    ReplyDelete
  3. pia Leila ni mrembo sana kuliko huyo Chiku mwenye kitambi, sijui Mzee Yusufu aliona nini kwa Chiku

    ReplyDelete

Top Post Ad