Pombe Zamzidi Gigy Money Alewa Chakari Ufukwe wa Coco

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Video Queen na Mtangazaji wa Runinga, Gifty Stanford ‘Gigy Money’ juzikati alifakamia pombe kali na kujikuta akilewa tilalila hadi kuzimika ndani ya klabu moja iliyopo kwenye Ufukwe wa Coco jijini Dar.

inti huyo asiyeishiwa na vituko alinaswa na mapaparazi wetu akiwa kwenye hali hiyo Jumatatu liyopita (Jumatatu ya Pasaka) ambapo awali alionekana akinywa pombe kali huku akivuta sigara. Baada ya kupombeka kwa muda mrefu huku akionekana kama aliyekuwa na mawazo mengi, taratibu mdada huyo aliyejaaliwa shepu alianza kupoteza ‘netiweki’.

Haikuchukua muda refu akawa amezimika na kuwaacha watu waliokuwa wakimuangalia wakimjadili kwa namna ambavyo alikuwa hajitambui. “Huyu bwana pombe zitamuua, mwenyewe huwa anasema anakunywa kidogo tu, sasa mbona leo hadi kazima, asipoangalia wahuni watamfanyizia,” alisema kijana mmoja aliyekuwa eneo la tukio.

Baada ya muda mfupi, alifika dada mmoja aliyeonekana kujuana na Gigy (inaonekana alipigiwa simu) ambapo alimchukua kwa kumkokota kisha akampakiza kwenye Bajaj wakaondoka.
Siku moja baada ya tukio hilo, Ijumaa lilimpigia simu Gigy Money na kumuuliza kulikoni amekuwa na tabia ya kulewa hadi kuzimika alipopatikana alijibu: “Ni maisha yangu, haina haja kunifuatilia.”
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. huyo Gigi anatafuta kiki tu si vingine alishapiga picha za nusu uchi, na alionyesha video ya nusu uchi na alishawahi kusema eti Ney wa mitego alimtongoza, wakati Ney wa mitego hana mpango nae na Ney wa mitego alisema live kuwa hamuoni Gigi kuwa ni mrembo, na kweli Gigi si mrembo ana tako tu lakini sura hana

    ReplyDelete
  2. muongo huyo hajalewa wala nini, ni kutafuta kiki tu

    ReplyDelete

Top Post Ad