TFF Yalaani Kitendo cha Mashabiki wa Simba Kuwarushia Mawe Viongozi na Wachezaji wa Simba Baada Kufungwa na Toto

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limelaani kitendo cha baadhi ya mashabiki wa mpira wa miguu kufanya vurugu mara baada ya mchezo kati ya Simba SC dhidi ya Toto Africans uliochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

TFF imesikitishwa na kitendo hicho cha mashabiki wa klabu ya Simba SC, na kusema inalaani kitendo hicho ambacho sio cha kiuana michezo, huku ikiwataka wanachama, washabiki kuheshimu viongozi wa klabu zao waliopo madarakani na kama kuna masuala ya kujadili wakayajadili katika vilabu vyao.

Mashabiki wa klabu ya Simba walifanya vurugu kwa kurusha mawe, wakilenga kuwadhuru viongozi wa klabu hiyo pamoja na wachezaji, magari waliyokuwa nayo baada ya timu yao kupoteza mchezo dhidi ya Toto Africans kwa bao 1- 0.

Jeshi la Polisi baada ya kuwasishi mashabiki kuondoka eneo la uwanja punde tu mchezo ulipomalizika, mashabiki hao walikaidi na kuendelea kurusha mawe hali iliyopelekea jeshi kutumia mabomu ya machozi kuwatanya katika eneo hilo.

Kufutia kitendo hicho, Jeshi la Polisi lilihakikisha bus la timu ya Simba SC na viongozi wake wanaondoka salama uwanjani baada ya kuwatawanya mashabiki hao, kwa kupitia mlango wa karakana ya wachina waliojenga uwanja huo.

Aidha TFF imeviomba vyombo vya Usalama na Ulinzi kuwachukulia hatua kali mashabiki waliohusika na kitendo hicho, kwani kufanya vurugu ni kosa la jinai na wanapaswa kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. na bado msemaji wao kutwa kuongelea timu za wenzie yanga na azam

    ReplyDelete

Top Post Ad