Wanajeshi wa Tanzania Waingia katika Kashfa ya ngono DRC ya Kuwaingilia Watoto Wadogo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wanajeshi Congo
Ujumbe wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo (Monusco) umeanzisha uchunguzi dhidi ya wanajeshi wa Tanzania wanaodaiwa kuhusika na vitendo vya udhalilishaji kingono.

Wanajeshi hao wanaodaiwa kufanya vitendo hivyo vya kingono dhidi ya raia ni wale wanaohudumu chini ya kikosi cha jeshi kilichopo Kijiji cha Mvivi karibu na mji wa Beni ulioko jimbo la mashariki mwa DRC la Kivu ya Kaskazini.

Monosco imesema imetuma mara moja timu ya uchunguzi katika eneo hilo kubaini ukweli wa kashfa hiyo inayowakabili Watanzania hao.


Monusco ilisema hatua za kinidhamu zitachukuliwa iwapo itathibitishwa kuwa wanajeshi hao walihusika katika unyanyasaji wa kingono ikiwamo dhidi ya watoto.


Shutuma hizo zinakuja baada ya wanajeshi wa Ufaransa na wa kutoka nchi nyingine kutuhumiwa kuhusika katika udhalilishaji wa kingono katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.


Umoja wa Mataifa (UN) umesema umesikitishwa na vitendo vya baadhi ya wanajeshi kufanya unyama kwa wananchi wa nchi hizo.


UN walisema kinachosikitisha zaidi wanaofanyiwa vitendo hivyo ni watoto wadogo.


----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad