Wifi wa Zari , Esma Platnumz Adaiwa Kutimuliwa Madale kwa Diamond Platnumz

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa
Hivi karibuni yalitua madai kwenye meza ya gazeti hili yakieleza kuwa, eti yule wifi nambari moja wa Zarinah Hassan ‘Zari’ anayefahamika kwa jina la Esma Platnumz (pichani) ametimuliwa pale nyumbani kwa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’, Madale jijini Dar na sasa anaishi Tandale.

Chanzo chetu ambacho kiliomba jina lake lisiandikwe gazetini kilidai kuwa, baada ya Zari kutua Bongo kabla ya kwenda Ulaya, Esma alitakiwa kufungasha kila kilicho chake na kwenda kuishi kwenye ile nyumba ya familia iliyokuwa ikikarabatiwa pale Tandale.


“Nyie mbona mnapitwa na ubuyu? Esma katimuliwa pale kwa Diamond, sasa hivi anaishi kule Tandale kisa ni zile figisufigisu zilizokuwa zikitokea kati yake na Zari.
“Diamond ameona ili mzazi mwenzake awe na amani, anayeweza kuondolewa kwenye ule mjengo aondolewe ili amani itawale na kusiwepo manenomaneno,” kilidai chanzo hicho.
Siku chanche baada ya ubuyu huo kunaswa, paparazzi wetu akiwa kwenye mishe zake alimuona Esma nje ya nyumba ya akina Diamond iliyopo Tandale huku akionekana kuwa, yupo maskani yake mapya.

Ili kupata ukweli wa madai ya kutimuliwa, paparazi wetu alimvutia waya Esma na alipopatikana alisema: “Nyie bwana, mimi ni wa kutimuliwa pale kwa Diamond? Huwa naishi pale na nikipenda ndiyo nakwenda Tandale lakini hayo mambo ya kwamba nimetimuliwa ili kumpisha Zari ajiachie na Diamond ni vijineno tu vya watu.”
_________

 Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. state house inaanza kuwatokea puani.

    ReplyDelete
  2. kwani huyo bibi kizee kaolewa hata atoe amri ya kuwafukuza ndugu wa Dai? au Domo kashainamishwa na umalaya wake woote kwishney.

    ReplyDelete
    Replies
    1. povu la kulilia dushelele hahah haya wamuita bi kizee na huyo mnayemuona mtoto mwenye shepu mbovu kuliko tembo, minyama tepetepe, kitambi cha gongo na kizazi kimekauka si over ajuza?!

      Delete
  3. esma we una shida ndoa yako umeivunja na sasa umebaki kumsumbua domo na bbikizee wake! ushindwe na ulegee.

    ReplyDelete
  4. ESMA UNATAKIWA UWE NA KWAKO BHANA,UTAISHIJE NA NA KAKA YAKO?

    ReplyDelete
  5. ww mwenyewe hapo juu unafugwa na kimada mbuzi kamba ww.

    ReplyDelete
  6. Esma wewe ni mtu mzima lazima uwe na kwako sio kuishi na ndugu, mimi mwenyewe nilikuwa na kwangu tangu nikiwa na miaka 18.

    ReplyDelete
  7. mstaarabike basi kidogo kwa kukaa na bi kizee wenu..achane utandale wenu huo...eti mi naishi pale...kwako?hata kama bi kizee hajaolewa si ana motto?tafuteni vyenu.amewakarabatia nyumba tandale..nini kumsongasonga?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad