Jerry Muro Amuomba Radhi Haji Manara

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

MKUU wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro amewaomba msamaha wapinzani wao, Simba na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa timu hiyo, Hajji Manara.
Kauli hiyo, aliitoa jana ambapo alisema amefuta majina yote aliyokuwa akiwaita Simba kama vile; Wazee wa Mchangani, Wazee wa Youtong, Wahapahapa, Chura na Wamatopeni baada ya Ligi Kuu Bara kumalizika na wao kutwaa taji hilo la ubingwa.

Muro alisema alifikia hatua hiyo kwa ajili ya kulinda ajira yake inayomruhusu kuongea chochote ilimradi asitukane.

Aliongeza kuwa, hayo maneno hayo yalikuwa ni chagizo na hayakulenga kumtukana wala kumkwaza mtu yeyote zaidi ni kuleta changamoto na ushindani.

“Naomba nichukue nafasi hii kuwaomba msamaha mashabiki wote wa Simba, pia rafiki yangu Manara kwa maneno na majina ya utani niliyokuwa nawaita wakati ligi kuu ikiwa inaendelea.
“Naomba nitangaze rasmi majina hayo sitawaita tena baada ya ligi kuu kumalizika.

“Pia ningependa kuwaaga akina Manara, Bwire (Masau) na Kifaru (Thobias) kuwa mimi hivi sasa ni wakimataifa, siyo levo yao tena ninakwenda kupambana na akina TP Mazembe timu nyingine tunazoshiriki nao Kombe la Shirikisho,” alisema Muro.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huyu mvuta bangi SIMPENDI...anasema hovyo kama chizi.....sijui kwanini hakufungwa jela kwa ile rushwa alokula kipindi kile.....mfyuuu, eti anaomba radhi....kamuombe radhi mkeo, mwaka wa 5 sasa hujampa mimba, uko bize na safari za yanga....tulia uzae!

    ReplyDelete
  2. Hapo juu hujui michezo wewe, huu mchezo hauhitaji hasira na dua zako mbaya zitakurudia mwenyewe huyu Muro anajua anachofanya then wewe lzm utakuwa mchawi tu humpendi umemuumba wewe???

    ReplyDelete
  3. Duh! Mbona nd'o kaharibu kabisaaaa. Mie nilikuwa siyajui majina yote hayo. Sasa nd'o kabisaaaa kanijuza! Huyu jamaa hatari kwa kuchomekezea, aisee!

    ReplyDelete
  4. Hakuna kufuta jina mpaka watakapokuwa wa kimataifa

    ReplyDelete

Top Post Ad