Mange Kimambi Hongera Sana Ujasiri wa Kuvalia Njuga Mambo Yenye Maslahi Kwa Taifa...

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Napenda kuchukua nafasi hii kumpongeza mwanadada jasiri asiyeogopa matokeo ya harakati anazofanya, ambazo nyingi zina maslahi kwa nchi yetu kwa ujumla wake.

Nafahamu kwamba kuna watu wengi tu wanamchukia huyu dada kwa tabia yake ya kuweka kila kitu wazi bila kujali madhara yake katika jamii au kwake yeye na hata familia yake.

Rejea madawa ya kulevya, na hata sasa alivyoamua kuacha kila kitu kikiwemo kile akipendacho UMBEA na kuweka maslahi ya Taifa mbele na zaidi akiungana na upinzani katika kuhakikisha kwamba Bunge linaonyeshwa live.

Hili la Bunge kutokuwa live lilionekana kwa watu wengi kama jambo zuri lakini hawa watu hawakujua ni kwanini serikali ilianza harakati hizi za kuminya haki ya kupata habari ambayo ni haki ya kikatiba kwa watanzania wote.

Hatahivyo, kati ya watu wachache waliojitolea kuungana na wabunge wa upinzani na wadau wengine ni huyu Mange Kimambi.

Mange, nakupongeza sana kwa ujasiri wako wa kukosoa yale yanayoonekana kuwa na matokeo chanya kwa jamii yetu in a long-run.

Hongera sana Mange na hongereni sana Wabunge wa Upinzani.

Japo mimi ni mwana-CCM, lakini nilikuwa ni moja kati ya watu waliokerwa sana na hatua ya Serikali kuingilia Bunge na hivyo kulikuwa na hatari ya Bunge kama Muhimili muhimu wa kuisaidia serikali katika kuendesha nchi kukosa nguvu na kuwa sehemu ya serikali.

Jambo hilo likitokea, basi tulipokuwa tunaelekea ni kubaya kuliko tulipotokea.

NARUDIA TENA, HONGERA SANA DADA MANGE KIMAMBI NA MUNGU AZIDI KUKUPIGANIA WEWE NA FAMILIA YAKO.

By JATELO1
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hongera Mange,siasa pembeni tuangalie maslahi ya nchi

    ReplyDelete
  2. Hana lolote Huyu kafulia uko marekani anataka nafasi ya uongozi na apati akipata basi ataishia kumwagiwa Tindikali Tu na Sisi tulioachwa uchi bila kosa.

    ReplyDelete
  3. Tatizo la Tanzania ni Elimu finyu ndo maana hata majirani zetu hutunyali hasa pale swala linapohitaji uelewa wa kielimu. Huyu binti anafaa sana kuwa mbunge wa upinzani wote waongee pumba zao. Moja, Bunge kuonyeshwa live ni vigumu kwani hatuna uwezo kipesa kulipia wenye satelight zao hatuwezi kuingia gharama hiyo kuwaonyesha wananchi utumbo wa hao wapinzani ambao wakiambiwa ati wabunge wadada wa ukawa wamechaguliwa aidha kupitia kanguo kadogo au undugu na viongozi wao wa ngazi ya juu, badala ya kusimama ndani ya bunge na kujieleza au kueleza walipataje kuteuliwa wanaamua kutoka nje ya bunge na kaka zao ni vilevile. Wamemchagua Katibu mtu muelewa sana sasa wanasema eti haongei lolote aongee utumbo??? Mwisho ni kwamba wapinzani Tanzania ni hatari kwa usalama na mshikamano wa TANZANIA, ona mtu hana pointi ya kuongea anaropoka tu eti Tanganyika inaikalia Zanzibar kwa mabavu mwenye kutoa kauli hiyo ni hatari sana haklafu ni kiongozi wa ngazi ya juu ya Ukawa mhhh. Ni JPM jinsi anavyowajibika imesababisha wapinzani kukosa cha kusema na hiyo ndiyo dalili ya kwanza ya kufa kwa upinzani. Kama wabunge wa upinzani wanataka kuonekana kwenye TV basi nafasi za kazi zipo EATV na CLOUDS hat Star TV but I'm sorry don't qualify.

    ReplyDelete

Top Post Ad