Video: Nisher alalamika kupoteza shilingi milioni 3.9 kugharamikia video ya Arosto ya G-Nako aliyoikataa na kuifanya tena na Hanscana

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Nisher analalamika kupoteza takriban shilingi milioni 3.9 kugharamia video ya wimbo wa G-Nako aliowashirikisha Nick wa Pili na Chin Bees ‘Arosto’ ambayo Warawara anadaiwa kuipotezea baada ya kutoipenda.
Nisher amefafanunua kwa kina kwa kupost video Instagram baada ya kubaini kuwa G-Nako aliirudia video hiyo na Hanscana na kuiachia jana.

Nisher anahisi kilichofanyika ni kama usaliti kwake baada ya kuweka nguvu nyingi kwenye video hiyo aliyoitarajia imrudishe kwa kishindo. Anasema baada ya G-Nako kudai ‘hajatisha’ kwenye video hiyo na kwamba ‘ni ya kawaida sana’, Nisher alimuomba kama vipi atoe fedha ili warekebishe makosa hayo.

Anadai Warawara alisema hakuwa na hela ya kufanya hivyo muda huo. Kutokana na uamuzi wa G kuachia video aliyofanya na Hanscana, Nisher ameamua kuitoa yake pia ili kuwapa uhuru mashabiki wahukumu kama kweli video hiyo ni mbovu.

Tazama video zote mbili hapo chini, aliyoongoza Nisher na ile ya Hanscana.

Chanzo:Bongo5
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mi sijui mziki sana lakn hanscana hebu abadilike yan mavideo yake yani rangi fulan hv unajua huyu ni hascana yanakuwa yame editiwa mnoo nadhani hicho ndo kitu watu sijui wanapenda...bt video ya nisher ipo poa labda colour yake tu imepoa...bt so far kwa mm nisiyependa makuu ya nisher ipo vzr mnooo has kwa nyimbo za ki gangster kama hizo...nyimbo za wabana pua lain lain ndo zinahitaji mirangi rangi

    ReplyDelete

Top Post Ad