Askofu Gwajima Mgonjwa, Kesi yake yapigwa Kalenda

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

PETER Kibatala wakili wa Josephati Gwajima Askofu wa Kanisa la ufufuo na uzima ameiomba mahakama kuhairisha tarehe ya kusikiliza kesi inayomkabili askofu huyo sababu anaumwa, anaandika Faki Sosi.

Kibatala amedai mahakamani Kisutu kuwa kutotokea kwa mteja wake leo kumetokana na yeye kuwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.

Wakili huyo mtaratibu mwenye hoja aliwasilisha madai hayo leo katika Mahakaama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Syprian Mkeha Hakimu Mfawidhi anayesikiliza kesi hiyo inayomkabili Gwajima

Mahakama imekubali ombi hilo na kwamba kesi hiyo itatajwa tena 2 Agosti mwaka huu.
Katika kesi hiyo Gwajima anadaiwa kutoa lugha ya matusi dhidi ya Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, Askofu wa Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Dar es Salaam.

Gwajima anadaiwa kufanya tukio hilo kati ya 16 na 25Machi, mwaka 2015 katika Viwanja vya Tanganyika Packers Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hivi gwajima ni mchungaji au mwanasiasa maana cmuelewagi kabisa au ndio kuuza majina vituko vituko vingi

    ReplyDelete
  2. Kesi IPO na inangoja mgonjwa apate afueni..lakini akirudisha namba hapo Labda ndiyo vile..la sivyo .....kila ukichelewa makali yanazidi..pole mchungwaji

    ReplyDelete

Top Post Ad