Babu Seya, Papii Wamwangukia Rais Magufuli

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

MWANAMUZIKI Nguza Vicking ‘Babu Seya’ na mwanaye, Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ ambao wanasota jela kwa kosa la kuwanajisi watoto 9, wamedaiwa kusaka uwezekano wa kujinasua gerezani kwa kumuangukia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli.

Taarifa kutoka kwa chanzo makini zimeeleza kuwa wanamuziki hao kwa kushirikiana na ndugu zao, wamemuandikia barua binafsi rais ili aweze kusikia kilio chao na ikiwezekana wasamehewe kutokana na mamlaka aliyo nayo.

“Si unakumbuka kipindi kile waliwahi kumuandikia waraka JK (Jakaya Kikwete, rais wa awamu ya nne) kumuomba awasamehe lakini bahati mbaya maombi yao hayakuzaa matunda! Wameona wajaribu kwa Magufuli ili ikiwezekana kupitia ile sheria inayompa mamlaka rais kusamehe mtu yeyote aliyehukumiwa kwa kosa lolote, awasamehe kina Babu Seya,

“Nasikia wameshaandika barua, wanaipeleka ikulu na wana imani Magufuli ni mtu anayeguswa sana na hofu ya Mungu, huenda akawasamehe,” kilisema chanzo hicho.

Alipotafutwa mtoto mkubwa wa Babu Seya, Mbangu Nguza na kuulizwa kama wamepeleka barua hiyo na matumaini ya ndugu zake kutoka gerezani, hakutaka kukubali au kukataa lakini akasema wao wana imani muda wowote ndugu zao watatoka gerezani.

“Kila siku nimekuwa nikisisitiza hili suala, labda niseme tena, Babu Seya na Papii watatoka siku si nyingi kutoka sasa,” alisema Mbangu.

Amani liliwasiliana na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa na kumuuliza kama wamepokea barua hiyo, alisema hawajaipata na kuomba apewe muda afuatilie na atatoa majibu.

“Sijaiona hiyo barua, ngoja nitafuatilia na nitakujulisha,” alisema Msigwa.

KUMBUKUMBU

Juni 25, 2004, Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam, Addy Lyamuya aliwatia hatiani Babu Seya na wanaye watatu, Papii Kocha, Mbangu na Francis.

Januari 27, 2005, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Thomas Mihayo alitupilia mbali rufaa yao iliyokuwa ikipinga hukumu hiyo.

Wakili wao, Mabere Nyaucho Marando akapeleka suala hilo Mahakama ya Rufaa Tanzania ambako Mbangu na Francis waliachiwa huru, Babu Seya na Papii wakaonekana bado wana hatia.

Babu Seya na wanaye walidaiwa kutenda makosa 10 ya kubaka na kulawiti watoto hao kati ya Aprili na Oktoba, 2003 katika maeneo ya Sinza ya Palestina, Dar es Salaam. Mpaka sasa wana miaka 12 gerezani.

Chanzo:GPL


----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. magufuli tunakuomba hawa watu hawakufanya haya kwa jamii, waaicgie watote inje halafu huone kama watafanya tena ukatili huu, lakini Rais waachie watoke nje kwani inawezekana hawajafanya hayo makosa, sababu ni raia wa nje ndiyo maana walifungwa, nakuomba rais waonee huruma hao mbona mmoja alifunguliwa na akatoka nje

    ReplyDelete
  2. jamani magufuli uwachie kwenye jamii hao watafanya mambo mazuri kwa jamii jamaani huenda hawajafanya makosa hayo ewe Mungu Magufuli wasamehe hao naona walisingiziwa

    ReplyDelete
  3. mimi nalia sana nikiwa jiji la Ulaya Magufuli hao hawakufanya makosa bali walisingiziwa, mzee Magufuli wasamehe hao viumbe vya Mungu kwani walikuja Tanzania kufanya kazi na walifanya kazi, nakuomba Rais Magufuli wasamehe hao kwani hawakuja Tanzania bila kukaa tuu bila kufanya kazi, walifanya, na hivyo vitu walisingiziwa kutokana walikuwa sio raia wa Tanzania

    ReplyDelete
  4. magufuli samehe hawa, huenda hawajanya hayo makosa wanakaa gerezani bure samehe hao watu kwani walikuwa ni wapiga kazi

    ReplyDelete
  5. MNA HAKIKA GANI KAMA HAWAKUFANYA???

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe hujui kitu funga bakuli lako kerbu wahedi wewe unaelewa kitu kinachoitwa kubambikiwa kesi wewe hao ndugu waliingia kwenye anga za wakuu adhabu yao wakabambikiwa hiyo kesi hujiulizi mwenyewe kesi ya kubaka hata kama kweli walitenda hilo kosa kwenda kufungwa kifungo cha maisha inaingia akilini mwako kweli?You better think twice before opening your mouth or shut the fuck up!

      Delete
  6. HAKUNA UHAKIKA KAMA WALFANYA,MAANA KWENYE HII KESI KULIKUWA NA STORY NYINGI.WASAMEHEWE NA WAENDE/WARUDISHWE KWAO.

    ReplyDelete

Top Post Ad