Chadema kutoa tamko zito Leo Ambalo Litarushwa na Vituo Vitatu vya TV

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), leo kinatarajia kulihutubia taifa kupitia vyombo vya habari vya ndani na nje kuhusu maazimio ya Kamati Kuu iliyoketi kwa siku nne mfululizo.

Maazimio hayo ambayo yanaitwa ‘mazito na makubwa’ kuwahi kutolewa na chama hicho katika siku za hivi karibuni, yanatarajiwa kuonyeshwa moja kwa moja na vituo vitatu vya runinga   nchini.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya chama hicho kimeeleza kuwa maazimio hayo ya Kamati Kuu yatatangazwa moja kwa moja kupitia baadhi ya vituo vya runinga  kutoa fursa kwa Watanzania kusikiliza maazimio hayo.

Kamati kuu ya Chadema imefanya kikao chake kwa siku nne mfululizo kikiwa kimeghubikwa na usiri mkubwa.

Taarifa ya chama hicho kwa vyombo vya habari jana, ilisema Kamati Kuu ilimaliza kikao chake cha siku nne jana na leo maazimio yake yatawekwa wazi kwa wananchi kupitia vyombo vya habari.

Taarifa hiyo iliyotolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Chadema, Tumaini Makene, ilisema kupitia mkutano huo yatatangazwa maazimio ya kikao hicho kilichohitimishwa    Dar es Salaam jana.

Taarifa hiyo ilisema Chadema kitatoa tamko zito la ukubwa wa aina yake.

“Licha ya mambo hayo chama kitatoa matamko mazito na makubwa ya aina yake ambayo hayajawahi kutolewa na chama chetu katika siku za karibuni."

Taarifa hiyo ilisema Kamati Kuu ilipokea taarifa ya kina juu ya masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na hali ya siasa nchini kwa sasa ambayo inatishia hali ya uchumi na ustawi wa jamii nzima kwa ujumla, hivyo taifa zima kuwa katika majaribu makubwa ya kukosa mwelekeo wa  uongozi.

“Kupitia mkutano huo, Chadema kitatoa mwelekeo wa hali ya nchi hasa wakati huu ambao taifa linaonekana kukosa dira ya uongozi kwa ajili ya ustawi wa Watanzania wote kwa ujumla” kilisema chanzo hicho ambacho hakikutaka kuwekwa wazi jina lake.

“Kupitia mkutano huo, chama kitazungumzia mipango ya kujiimarisha kuendelea kuwatumikia wananchi na kusimamia dira ya mabadiliko na uhuru wa kweli nchini,”alisema Makene.

Alipoulizwa kuhusu taarifa hizo, Makene alisema suala hilo halijathibitishwa rasmi kama mkutano huo   utaonyeshwa moja kwa moja katika runinga.

“Hata mahali utakapofanyika mkutano huo bado hapajajulikana, nitakupigia simu kesho asubuhi (leo) kukujulisha wapi tamko hilo litatolewa."  Alisema

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. HAPA KAZI TU.

    ReplyDelete
  2. Huo utakuwa sio mkutano wa kisiasa?
    Ngoja tusikilizie.

    ReplyDelete
  3. Hawana jipya hao nao, hayo matamko yao ya 'kususia susia' tumeshayazoea......mara hatumtambui Raisi, mara hatuingii bungeni, mara hatunywi maji, mara hatuogi, mara hili mara lile hahahah wanachekesha walonuna.... Labda mkijinyonga ndio litakuwa jipya, vinginevyo JPM ndio habari ya dunia kwa sasa..........CCM mbele kwa mbele...MUPO!!??!!

    ReplyDelete
  4. Mna taabu sana!!!! wenzenu tulisomea medicine kuepuka kuishi maisha ya kugushiii heeeheeeeee

    ReplyDelete

Top Post Ad