Kitwanga afunguka kuhusu kutumbuliwa na Rais Magufuli Pamoja na Uhusika wake Katika Sakata la Lugumi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge wa jimbo la Misungwi, Charles Kitwanga (CCM) amezungumzia jinsi alivyopokea kutumbuliwa kwake na Rais John Magufuli ambaye anaamika kuwa rafiki yake akisema hawezi kuhoji uamuzi huo.

Kitwanga aliwaaambia waandishi wa habari nyumbani kwake Misungwi kuwa ingawa hawezi kuhoji uamuzi huo, kuna kundi kubwa la wauza madawa ya kulevya ndio waliolikuza tukio hilo kwa lengo la kumchongea hadi kuondolewa kwenye nafasi hiyo.

“Anayofanya Dk. Magufuli nampongeza sana kwani ni mtu ambaye namfahamu. Ni mwadilifu, msikivu, namshukuru kwa kuniamini kufanya kazi naye katika Serikali yake hivyo siwezi kuhoji alichoamua kwa sababau aliyetoa ndiye aliyeondoa,” alisema Kitwanga.

Katika hatua nyingine, Mbunge huyo wa Misungwi alikana kuhusika kwa namna yoyote katika sakata la kampuni ya Lugumi Enterprises Ltd iliyopewa zabuni ya kufunga mashine za kutambua alama za vidole kwenye vituo vya polisi nchini, na kudaiwa kulipwa kiasi kikubwa cha fedha wakati kazi haikufanyika kama ilivyotarajiwa. Sakata hilo bado lipo katika uchunguzi japo dalili za kujadiliwa bungeni zinaonekana kufifia.

“Rais wa Kwanza wa Tanzania hayati Mwalimu Julius Nyerere, kuna wakati alituhumiwa akidaiwa kuwa na mpango wa kumpindua Rais wa Kenya baada ya kuzuru nchini humo. Alipoulizwa na waandishi wa habari alijibu, ‘hivi mtu akikwambia mimi ni mume wa mama yako utakubali?’, sasa hilo ndilo jibu langu kwa Watanzania ili wasiniulize tena,” alisema Kitwanga.

Akizugumzia umiliki wa kampuni ya Infosys, alisema kuwa yeye ni mwanzilishi tu wa kampuni hiyo na hivi sasa inamilikiwa na mwanae baada ya kumuuzia asilimia 33 ya hisa zake na kwamba taarifa ya mauzo hayo ziko wazi.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Sawa, lakini ni ngumu kumeza - kwamba aliuza hisa 33% kwa wachache wataafiki ila wengi tutabaki kukataa. Pongezi kwa kuwa anatambua kwamba Mhe. Magufuli ni mwadilifu

    ReplyDelete
  2. Hapa mbona inachanganya? Huyo ni Kitwanga au ni Lugumi?

    ReplyDelete

Top Post Ad