Mtangazaji mahiri wa kipindi cha Jahazi cha Clouds FM, Gadner G Habash amekanusha kumdhalilisha aliyekuwa mke wake Lady Jaydee kupitia video ambayo ilisambaa katika mitandao ya kijamii miezi michache iliyopita.
Gadner
Akiongea na Bongo5 Jumamosi hii, Gadner amesema anaheshimu faragha ya muimbaji huyo wa wimbo ‘Ndi Ndi Ndi’ na kamwe hawezi kufanya kitendo kama hicho.
“Kusema kweli sitaki kulizungumzia suala la Lady Jaydee, naheshimu faragha yake,” alisema Gadner. “Ile issue ilikuzwa na mitandao ya kijamii, na mitandao ya kijamii inajua kutengeneza mambo hata yasiyokuwepo,”
Mtangazaji huyo amesema hana tatizo na mwanadada huyo kwa kuwa kila mtu alisha ‘move on’ na anaendelea na mambo yake.
Katika video ambayo ilisambaa mitandaoni, Gadner alisikika akisema “Na sina neno na yule mtoto wa kike. Nimeshamkojoza kwa miaka kama 15 hivi,” kauli ambayo ilichukuliwa vibaya na watu wengi.
Chanzo:Bongo5
Sikumdhalilisha Lady Jaydee Kwenye Video iliyosambaa Mitandaoni – Gadner
6
July 14, 2016
Tags
boya wewe gadna,unafikiri unaongea na nani?ata mtoto mdogo anaelewa ulikuwa unamaanisha nini kama siyo kumdhalilisha.
ReplyDeleteNimesoma na mwanae,ninamuheshimu sana lakini kwa neno lile hata mimi nilikereka sana jamani.Mungu amsaidie maana kwa jinsi anavyoongea ni kama kagundua kuwa alifanya kosa.Tumsamehe.
DeleteUle usemi wa mtu mzima ovyo unawahusu wote. JD naye pia alimprovoke na ndi ndi yake. Hapo ngoma draw.
ReplyDeletehata jidee hakumaanisha kumuimba Gadna kuwa yeye ni chizi asopona.
ReplyDeletehahaha utaisoma mwenzio amepata mzungu mwenye kumjali.ndi ndi ndiiiiii.
ReplyDeleteunajitetea tu hakumtendea hakikabisa!!!!
ReplyDelete