KIMENUKA..Kauli ya Paul Makonda ya Kutaka Polisi Iwapige watu Wakiwakuta Msituni Yasababishwa Aitwe na Tume za Haki za Binadamu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imesikitishwa na matamshi ya Mhe. Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam yanayokiuka misingi ya utawala bora aliyoyatoa tarehe 25 Agosti, 2016 wakati wa kuaga miili ya askari Polisi watatu waliouawa Mbande, Mkoani Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Tume, Mhe. Bahame Tom Nyanduga, leo (Agosti 26, 2016) Mhe. Makonda ametumiwa barua ya wito inayomtaka afike makao makuu ya Tume mtaa wa Luthuli, tarehe 30 Agosti, 2016 ili kujadili kile Tume ilichokiona kuwa ni kejeli kwa Tume pamoja na jumuiya yote ya watetezi wa haki za binadamu.

Aidha, Tume imeona kuwa maagizo aliyoyatoa Mkuu huyo wa Mkoa kwa Jeshi la Polisi hayana msingi wa kisheria na hayako ndani ya mamlaka ya Mkuu wa Mkoa.

Kwa mujibu wa Kifungu cha 6(1)(f) na (i) pia Kifungu cha 27(1) na (2) (a) vya Sheria ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Sura Na. 391 ya Sheria za Tanzania 2002, THBUB ina mamlaka ya kuchunguza mwenendo wa mtu au taasisi yoyote kuhusiana na utendaji wa kazi zake zinapokiuka mipaka ya madaraka yake, ili kuchukua hatua za kurekebisha ukiukwaji huo.

Imetolewa na:

(SIGNED)
Idara ya Elimu kwa Umma na Mafunzo

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Agosti 26, 2016
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hili jipu lazima uma ulitumbueteba haraka
    Tulisena kuwapa vyeo watoto wadogo hii ndo faida yake
    Anaropoka tu
    Hivi Tanzania hakuna watu kuwafundisha viongozi jinsi ya kuongea kwenye media
    Hata jinsi ya kukaa kwenye media?
    Old is gold

    ReplyDelete
  2. Nafikiri huu utumbo wa haki za binadamu TANZANIA ni upuuzi wa hali ya juu
    Hivi ni nani aliruhusu huu upuuzi uwe established Tanzania??? Alifanya kosa kubwa sana
    Watanzania ni malimbukeni hawakuhitaji huu upuuzi wa haki za binadamu kwani hawajui nini maana yake wala kazi zake kwani mwisho watadai watuhumiwa walevi wapelekewe bia Segerea au Keko
    Hivi si CHADEMA hawa??? mbona wako sana kutetea wahalifu na wezi???? Sijasoma wakitetea walikatwa mishahara yao visivyo ila wakwenda sambamba na UKAWA au CHADEMA
    Tanzania mhalifu auawe iwe kwa moto au vyovyote vile kisha haki za binadamu pigeni kelele au itabidi muwe victimised kwanza ndo mjue nini mnatetea maana mzigo alobeba mwenzil ni kama kifurushi cha pamba au siyo???
    Mhalifu piga ua tu na ndio mwendo siyo kubembeleza MWISHO,, Mhalifu mvishe tairi kisha washa motooooo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe mpumbavu na mjinga kama huyo unaye mtetea
      Tunaishi dunia ya uwazi na ukweli
      Ukiona kiongozi hataki
      Ushauri
      Wala kukosolewa
      Huyo ni dikteta tena uchwara
      Au mpuga mapepe
      Yaani chuya
      Fyuuuuuu

      Delete

Top Post Ad