Mbowe: Mpango wa kuhamia Dodoma ni wa kukurupuka

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema hakitotekeleza mpango wa kuhamia Dodoma kwani ni wa kukurupuka.

Msimamo huo umetolewa jana na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe alipozungumza na gazeti hili wakati wa kutoa heshima za mwisho za aliyekuwa mpigapicha mwandamizi wa gazeti la Tanzania Daima, Joseph Senga ambaye anatarajiwa kuzikwa leo huko Kwimba, Mwanza.

“Serikali inaendeshwa kwa kukurupuka. Ni mpango usiotekelezeka,” alisema Mbowe.

Alisema uhamaji unaotekelezwa sasa haukuwa na maandalizi wala mkakati kwenye ilani ya chama tawala wala Bajeti ya Serikali hivyo kuwa na uwezekano mkubwa wa kukwama huko mbele.

Miongoni mwa vitu vinavyoufanya mpango huo usitekelezeke kwa ufanisi, kwa maoni yake, alisema miundombinu ya kutosheleza watendaji wote na wadau wengine muhimu ambao watalazimika kufuata huduma muhimu za wizara na idara za Serikali.

“Huku ni kuwaumiza wananchi. Watumishi wa Serikali, wanahabari na wadau wengine wakihama wote watapata wapi malazi katika mji ule?”

Muda mfupi baada ya kukabidhiwa majukumu ya kuiongoza CCM, Julai 23, Rais John Magufuli alieleza nia yake ya kutekeleza uhamisho wa makao ya Serikali kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma na kwamba atahakikisha, ndani ya miaka minne anatimiza ndoto hiyo ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ya tangu mwaka 1973.

Siku moja baadaye, akihutubia kwenye hafla ya Siku ya Mashujaa mjini Dodoma, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alitangaza kuhamia mjini humo Septemba na kusema kuwa wizara nyingine zitamfuata.

Tangu kutolewa kwa matamko hayo ya viongozi waandamizi wa Serikali; wizara, taasisi, mashirika ya umma, idara na baadhi ya ofisi binafsi, mabalozi na wanadiplomasia zimeanza kuandaa mazingira ya utekelezaji huo.

Lakini, Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni alionyesha wasiwasi wake juu ya umakini wa Serikali kutekeleza azma hiyo akisema kutakuwa na usumbufu mkubwa kwa watumishi na familia zao suala linaloweza kupunguza morali yao ya kazi. “Watu wana familia zao. Watoto wanasoma... Dodoma hakuna shule za kutosha watoto watakaohama na wazazi wao.”

Alisema wakati wazo hilo linatolewa na kuungwa mkono enzi za Mwalimu Nyerere kulikuwa na sababu za msingi lakini hivi sasa kuna mabadiliko makubwa yaliyochagizwa na maendeleo ya sayansi na teknolojia. Alisema wakati huo mindombinu ya mawasiliano haikuwa rafiki tofauti na iliyopo sasa inayowezesha watu walioko New York, Marekani kufanya mkutano na wenzao waliopo popote duniani kwa kutumia miutano kwa njia ya masafa. “Sababu zimepitwa na wakati,” alisisitiza.

Alishauri, mpango huo ungetekelezwa kwa utaratibu maalumu, akitoa mfano kwa wizara moja au mbili kuhama kwa kila mwaka mpaka zitakapokamilika ili kupunguza gharama zisizo na ulazima.

Alisema kuhamisha wizara siyo waziri au katibu mkuu pekee, bali ni watumishi wote na miundombinu yote iliyopo ambayo ni muhimu kwa utekelezaji wa majukumu yake: “Kwa mfano, Wizara ya Kilimo ina watumishi 2,000 na maelfu ya mafaili yenye taarifa za kiutendaji… unawahamishaje watu wote hawa na mindombinu iliyopo unaifanyaje? Namshangaa IGP anaposema anahama wakati mifumo yote ya uchunguzi na taarifa imejengwa hapa kwa kutumia mabilioni ya fedha za wananchi.”

Wiki iliyopita, Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa Polisi, Nsato Marijani alisema jeshi hilo litahamia Dodoma mwezi huu na watakaohusika ni Inspekta Jenerali na baadhi ya makamishna.

Chanzo: Mwananchi
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

12 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. KWELI KUNA WATU NA VIATU,ILA WEWE KUBADILISHA GIA ANGANI ILIKUWA NJEMA?NA MBOWE HAITATOKEA HATA SIKU MOJA ASIFU JITIHADA ZA RAIS JPJM,NI MTU WA CHUKI TU NA MAPOVUUUUUUUUU----
    WAKATI WENZIO WA VYAMA PINZANI PIA WANASIFU TULIJUA WEWE LAZIMA UTAPONDA,KWANI MBONA HATA MAGUFULI ALIVYOANZA KASI YAKE WEWE ULISEMA KILA ANACHOFANYA ANAIGA SERA ZA CHADEMA.

    ReplyDelete
  2. Yetu macho
    Mafuta mafuta hayo

    ReplyDelete
  3. sawa kuhamia dodoma, alakini si kwa mda mchache. kuna mambo mengi ya kuandaa. popole, si kwa speed ya michael chumacher wa formuler one.

    ReplyDelete
  4. Huyo ndio Mboe Raisi wa Chadema 2020,,,Hama zuri kwake kila lifanywalo na Serikali ni batili,,,,Huna sera niliipenda sana Chadema lakini sasa hivi bora kukaa bila chama wizi mtupu.

    ReplyDelete
  5. Jamani achani wahame it is long over due.Maana wakisema pole pole itakuchukua miaka 40.Waende foleni ipungue.

    ReplyDelete



  6. miundombinu kwanza ndo unahamisha watu mwenyekiti apunguze mbwembwe kwanza

    ReplyDelete
  7. kuhamisha wizara zote kwa mara moja haiwezekani kama wengi mnavyofikiri ni gharama kubwa sana na kama huikuwekwa kwenye bajeti hapo ni kukurupuka na kwanini kama walikua na mpango wa kuhamia Dodoma wasingetengeneza miundo mbinu tangu siku nyingi hatukatia kuhamia Dodoma ila sio swala la mwezi mmoja na wakati kuna mambo yanahitaji utekelezaji wa haraka kama maabara na miundo mbinu ya hospitali vijijini

    ReplyDelete
  8. Serikali mpya umejaa wasomi
    Maprofessa
    Ma dr
    Ma ingineer
    Kila kona ya nchi
    Yetu nacho

    ReplyDelete
  9. Hata hiyo kauli ya Mbowe ni ya kijinga na kakurupuka vile vile. Mwalimu nyerere alitamani ndani ya maisha yake akiona serikali ikihamia dodoma sasa tulitegemea kiongozi mwenye akili timamu kusema yakwamba tumechelewa kuchukua maamuzi ya kuhamia dodoma badala yake mtu anatema pumba. Na ndio maana tunasema nchi hii itapiga hatua za maendeleo kwa haraka chini ya Magufuli.

    ReplyDelete
    Replies
    1. umenena na hicho cha maendeleo ndo tunachokisubili toka kwa JPM mengine ni majungu

      Delete
  10. POVU NA MATE SASA..............MIE KANDOOOOOOOOOOOOO

    ReplyDelete
  11. Kukurupuka kulikovunja rekodi ni UKUTA. Zaidi ya hapo sijaonaaaa, Mr Mboooe!

    ReplyDelete

Top Post Ad