Mzee Yussuf Ataendelea Kusikika Japo Anasema Amestaafu Muziki - Khadija Yusuf

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Zikiwa zimepita siku kadhaa tangu Mzee Yussuf kutangaza kuacha rasmi kazi ya muziki na kumrudia Mungu, mdogo wa mzee Yussuf, Khadja Yussuf ambaye ni muimbaji katika bendi ya Jahazi Modern Taraab amefunguka na kusema Mzee Yusuph lazima atasikika.

Khadja Yussuf
Amesema kuwa licha ya kaka yake huyo kuacha muziki lakini 'band' hiyo itaendelea kufanya kazi ya muziki na wataendelea kutoa kazi ambazo Mzee Yussuf alishiriki.

Akiongea kwenye kipindi cha eNewz ya EATV Khadja alisema kuwa ni kweli mzee amemrudia Mungu lakini jambo hilo haliwazuii wao kuendelea na kazi ya muziki na kudai Mzee Yussuf atake asitake lazima katika baadhi ya kazi ambazo tayari alishafanya kwenye bendi hiyo ataonekana tu kwani hawawezi kufanya marekebisho na kumuondoa katika kazi hizo ambazo zinatarajiwa kutoka siku za karibuni.

"Hata kama Mzee amemrudia Mungu muache huko huko na Mungu wake, lakini sisi tutaendelea kufanya kazi na kutoa kazi nzuri zaidi hata ya hizo, kwani waimbaji wapo wengi siyo mzee tu, nachoweza kusema ni kwamba kuna kazi ambazo tulishafanya na Mzee Yussuf nyingine amepiga kinanda kwenye wimbo wa mkewe, na nyingine ameonekana au ameimba, hizo kazi zitaendelea kutoka, tunachoweza kufanya tunaweza kuondoa picha yake kwenye band lakini kazi ambazo ameshiriki lazima ataonekana tu zitakapotoka hilo hawezi kulikwepa" alisema Khadja Yussuf
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ulimi ni kitu kidogo sana lakini madhara yake ni makubwa sana inategemea na jinsi unavyoutumia kama ni Kheri au Shari!!!

    ReplyDelete
  2. Duuu huyo Khadijah haya zilishakutupa mkono. ..eti yeye na Mungu Wake..Duah...kitu kingine cha kushangaza,ni vipi band ni mali yako kisha uiache iendelee kutumika ktk magh'si .

    ReplyDelete
    Replies
    1. Anasema mwache na Mungu wake ina mana kuwa yeye hana Mungu. Ajuwe Mungu yuko na siku itapoadia ndipo atapomjuwa. Kwanza aitazame hali yake

      Delete
  3. hongera mzee Yusuf kwa kujitambua kabla hujafumba macho.wengi wetu hatujui kwa nini tumeumbwa...umemjua,umempenda,na umeamua kumtumikia Mungu...hongera kwa busara hiyo.

    ReplyDelete

Top Post Ad