Njemba Avamia Makao Makuu ya Trump, Adakwa!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

NEW YORK: Njemba mmoja nchini Marekani aliyejiita kuwa ni mtafiti binafsi na shabiki wa Donald Trump, jana Agosti 10, 2016 alitumia masaa matatu kupanda jengo la mfanyabiashara huyo maaufu duniani ambaye pia ni mgombea urais wa nchi hiyo kwa tiketi ya Chama cha Republican lililopo jijini New York.

Taarifa zimeeleza kuwa njemba huyo mwenye umri wa miaka 21 mkazi wa Virginia alitumia vifaa maalum kupanda ghorofa hilo lililojengwa kwa vioo ambalo pia ni Makao Makuu ya Kampeni za Bwana Trump na ndiyo Makao yake Makuu Kibiashaa kabla ya polisi kumtoa akiwa amefikia ghorofa ya 21 huku akiwa amechomwa vibaya na vioo vya jengo hilo.

Trump anaishi kwenye ghorofa ya ya juu kabisa ya jengo hilo lakini kwa sasa anafanya kampeni zake nje ya mji.

Mpandaji alijivuta huku akiwa akionekana kuwa amelewa, akitaka kuingia ndani ya jengo hilo. Polisi waliofika eneo la tukio wamesema hawakuweza kutambua nini haswa lilikuwa lengo lake.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kapagawa na sera za mzee trump za kuruhusu watu kuruhusiwa kununua silaha bila longo longo! ha ha ha haaaa

    ReplyDelete

Top Post Ad