Kuahirisha Ukuta, Polisi Wapumua

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

JESHI la Polisi limepumua baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuahirisha mikutano na maandamano yao, anaandika Pendo Omary.

Hatua ya kuahirisha mikutano na maandamano iliyotangazwa kufanyika chini ya mwavuli wa operesheni ya Umoja wa Kupinga Udikteta (Ukuta), imepongezwa na Simon Sirro, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

Kulikuwepo na vuta nikuvute kati ya Chadema na serikali kuhusu Ukuta hivyo kuzua taharuki na hisia za kutokea machafuko iwapo juhudi za kutafuta suluhu zingeshindikana.

Maandamano hayo yalitarajiwa kuanza kufanyika kesho lakini leo Freeman Mbowe, mwenyekiti wa chama hicho ametangaza kusitisha kwa kile kilichoelezwa, uchaguri wa taasisi mbalimbali nchini ikiwa ni pamoja na kuisha mazungumzo ya taasisi hizo na Rais John Magufuli.

“Nawashukuru sana viongozi hawa kwa uzalendo waliouonesha kwa kusimamisha mikutano na maandamano yao.

“Ila kuhusu kesho, wananchi wasishangae kuona magari yetu yakipita barabarani wakajiuliza kulikoni wakati Chadema wametangaza kutoandamana. Sisi kama Jeshi la Polisi bado tupo kwenye oparesheni zetu za kupambana na wahalifu,” amesema Siro.

Aidha, Sirro amesema oparesheni inayoendeshwa na jeshi hilo katika Mikoa ya Pwani na Dar es Salaam inaendelea vizuri na mpaka sasa tayari linawashikilia watuhumiwa zaidi ya 20 baada ya kufanya msako mkali.

“Watu zaidi ya 20 wamekamatwa. Wengi wanaeleza namna wanavyolifahamu tukio (mauaji ya askari wanne), lakini wengine ni wahusika katika matukio mengine ya uharifu. Ukamataji bado unaendelea katika maeneo ya Vikindu na Dar es Salaam,” amesema Sirro.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Chadema imekosa dira badala Dr Slaa kuondoka sasa hivi wanaibuka na mikakati hovyo hovyo isiyo na tija kwa mwananchi watu wanatafuta wajikimu maisha sio kupoteza muda na siasa njaa hakuna mtanzania aliyekuwa mburula akafuata mambo ya kijinga na matukio yasiyo na mshiko unategemea watu waingie mitaani kuandamana kisa kesama Mbowe kawa nani anataka kujifanya nae ni serikali hakuna serikali ndani ya serikali

    ReplyDelete
  2. ULISHAWAHI ONA POLISI WANAPUMUA/KUPUMZIKA?SAA ZOTE WAKO KAZINI,NA WANAKULINDA WEWE NA FAMILIA YAKO USIKU NA MCHANA.SEMA"POLISI HAWAJARIBIWI"

    ReplyDelete
  3. Hongera saana mheshimiwa Mbowe kwa kuonesha uzalendo wake kwa watanzania. mungu ibariki tanzania

    ReplyDelete
  4. Hivi jeshi kama hilo lingekutana na wananchi wanao andamana ingekuaje!!? bora Chadema walivyoacha kuandamana maana hayo mazoezi ya mwezi mzima ingekuwa shida. Ila ni bora wangeungana na
    JWTZ kufanya usafi.... maana kusudi limepotea..

    ReplyDelete
  5. Simpendi huyu Siro
    Kama Hitler
    Pumbavu sana huyu
    Utatumbua

    ReplyDelete

Top Post Ad