RAIS Magufuli: Tetemeko Halijaletwa na Serikali, Watu Wafanye Kazi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mkuu Anasema waathirika wasikae tu huko wanangoja hela za serikali kwa sbb wanasikia zimechangwa,waanze kujisaidia kwanza wao na serikali itawasaidia pale waliposhindwa.

Mkuu anasema mtu ukuta umedondoka, anataka asubiri serikali ndio imtengenezee! Watu wajue tetemeko ni janga la asili halijaletwa na CCM. Waanze kwa kujenga wenyewe kuta zilizodondoka sio wasubiri serikali, sababu maisha yanendelea na watu wanatakiwa wafanye kazi kwa kujenga nyumba zao na sio kila kitu serikali itafanya.

Na wale wanasiasa wanaotaka kutumia janga hili kujinufaisha kisiasa mkuu anasema waache mara moja....Na kasema wote wanaotumia janga hili kukusanya misaada kwa njia ya kitapeli, basi wakamatwe mara moja.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Serikali hii ni masikini Serikali ya Chadema ingetoa shilingi bilioni moja kwa kila muathirika kwani sio wengi sana na chama kina pesa za dharura kama hizi,,, matrilioni ya shilingi na madolari yasiyohesabika

    ReplyDelete
    Replies
    1. Dah Chadema imekuwa tajiri kabla yakushika serikali je ikishika serikali si itakuwa balaa michongo mbele kwa mbele tutakula milo sita kwa siku

      Delete
    2. Koma mwana kukoma mtoto wa haramu wewe usiyejuwa baba yako
      Umezaliwa labda kipindi cha bunge Dodoma wakati wa mbio za mwenge au
      Kwenye mikutano ya CCM
      Wakati mama yako akitararika kutafuta riziki
      Mtoto mwenye malezi na adabu
      Hawezi kusema Kama usemayo

      Delete
  2. Tujifunze na kuuelewa mtu asemacho
    Kiswahili kigumu watanzania tumezoea yahe yahe nyingi
    Tukubali ukweli
    Wazungu wameendelea kwa lugha hii
    Ya moja kwa moja
    Thanks John

    ReplyDelete
  3. Mungu apishe mbali lakini kama janga ili ua zaidi ya ili likitokea serikali ipo tayari?? Mungu atubari na poleni sana wana Kagera

    ReplyDelete
  4. alijinadi kaletwa na Mungu, akazindua push up KAGERA, leo anawambia wasitegemee serikali wafanye kazi na yeye amechaguliwa kwa wanyonge leo vipi Mungu si wa kuchezewa

    ReplyDelete
    Replies
    1. kwani yeye magufuli ndo kaleta tetemeko?? kachaguliwa na wanyonge wa tz nzima na sio eneo moja tu, kaletwa na Mungu ndio na ndo maana kauli zake ni za wazi hazina kuficha ficha. Watu mmezoea kudanganywa kiasi kwamba ukweli kwenu ni kosa la jinai. MSEMA KWELI MPENZI WA MUNGU mtabaki kulalamika lakini ukweli ndo huo fanyeni kazi serikali ni ya watu wote kuna wengine sasa hivi wana janga la njaa nao wadai serikali, wagonjwa, mafuriko, ukame n.k.

      Delete
  5. DAAAAA...maneno makali sana.mimi kama mzazi nimesikia mpaka tumbo linauma...hata kama ndio ukweli...Mungu atuhurumie.Tunafundishwa kusaidiana...wananchi tuwachangie wenzetu...tuone sura ya Mungu kwenye wahitaji hawa maana ataenda kutuambia..nilikuwa uchi ukashindwa kunivisha..nilikuwa na kiu ukashindwa kuninyeshwa..nilikuwa na njaa ukashindwa kunilisha...wangekuwa na uwezo huo wasingekubali kupigwa baridi siku zote hizi..

    ReplyDelete

Top Post Ad