Tundu Lissu Aponea Chupuchupu Dhamana Yake Kufutwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Hofu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kumfutia dhamana Tundu Lissu ambaye ni mtuhumiwa wa kesi ya uchochezi, imetoweka baada ya mahakama hiyo kukubaliana na utetezi wa  wadhamini wake kuwa, Lissu yupo Ujerumani kwa matibabu.

Lissu ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa jimbo la Singida Mashariki, alishindwa kuhudhuria mahakamani siku ya juzi na hivyo wadhamini wake kutakiwa kufika mahakamani jana kujieleza, kwanini mtuhumiwa huyo asifutiwe dhamana.

Kesi ya uchochezi inayomkabili Lissu ni kesi Na. 208 katika gazeti la MAWIO akiwa ni mtuhumiwa namba nne sambamba na Jabir Idrissa, Simon Mkina, na Ismail Merhaboob.

Jabir ni mwandishi mwandamizi wa MAWIO, Mkina ni mhariri wa gazeti hilo na Merhaboob ni meneja wa kampuni ya uchapishaji magazeti inayojulikana kwa jina la Flint.
Jana, wadhamini wa Lissu Ibrahim Ahmed na Robert Katula walisimama mbele ya Hakimu Thomas Simba anayesimamia kesi hiyo, na kusema kuwa Lissu hakutokea  mahakamani kwa sababu amesafiri nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.

Hata hivyo, upande wa mashitaka ukiongozwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali Mutalemwa Kisheruji uliiomba mahakama kuzuia hati ya kusafiria ya mshitakiwa Lissu pamoja na kumuwekea sharti la kuiomba mahakama kibali cha kusafiria endapo atarudia tena kosa hilo kutokana kwamba hakufuata sheria kwa sababu alitakiwa kutoa taarifa mapema kabla ya siku ya shtaka kusikilizwa.

Lakini Hoja hiyo ilipingwa na Wakili wa upande wa utetezi Peter Kibatala na kuiomba mahakama kutenga siku nyingine ambapo alimuahidi hakimu kuwa kosa hilo halitajirudia tena na siku husika ya kusikilizwa shitaka mshatikiwa atakuja mahakamani.

Baada ya kusikiliza maombi ya pande zote mbili, Hakimu Simba alitoa onyo kali kwa mshitakiwa na kuwaambia wadhamini wa Lissu kuwa, endapo siku nyingi mshitakiwa huyo hatakuja mahakamani, wadhamini watalipa dhamana.

Hakimu Simba aliahirisha kesi hiyo hadi Oktoba, 4, 2016 baada ya mawakili wa pande zote mbili kuiridhia tarehe hiyo iwe siku ya kusikilizwa shtaka hilo.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Lissu, usiichezee Mahak,ama. Hati yako ya kusafiria itahifadhiwa mahali husika na Jina lako litawekwa on ontrolled List. Na usirudie mkosefu wa Amani na Afya Inalega lega, Bado unautaka uwana saiasa Uchwara!!! Hapa Kazi Tu .. Mtanyooka.

    ReplyDelete
  2. Huu ni wakati muwafaka Kuwashikilia Waliompatia Dhamana, Mpaka atakaporipoti Mtuhumiwa na itakuwa ni somo ili Asidharau Mahakama na sheria zilizopo. Anadhihirisha Ukosefu wa Nidhamu ya Hali ya juu na kutojali Mahakama. Waliotia Zaamana Washikiliwe Lumande .

    ReplyDelete
  3. Lissu ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu ( Kwa Hiyo ndiyo avunje sheria? ) Itabidi apewe somo ili afate sheria. Jina lake liwekwe Airport na akiyua ni kituoni na mbele kwa mbele Mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake na Kosa la kuondoka nchi bila Taarifa linaongezeka ambalo pia anahitaji kulijibu. na alipaswa kujulisha Mahakama kabla ya Kuondoka kama anavyo dai.

    ReplyDelete

Top Post Ad