Mr Nice Azungumzia Tetesi Kuwa Ana Ugonjwa wa Ukimwi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Gazeti la Taifa Leo la nchini lilifanya mahojiano na msanii mkongwe wa muziki wa Tanzania Mr Nice. Katika moja swali ambalo aliulizwa ni kuhusu tetesi ambazo zimesambaa nchini humo kuwa ana HIV.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya muziki wake nchini Kenya, alikanusha uvumi huo huku akieleza nini kilimkuta mwaka jana mpaka akalazwa hospitali kwa miezi kadhaa.

“Kaka wewe mwenyewe ukinicheki nilivyo fresh nina ngoma kweli?,” Mr Nice alimuuliza mwandishi huyo huku akicheka. “Siugui Ukimwi lakini ni kweli mwaka jana nililazwa hospitali kwa miezi mitatu kuanza October. Nililishwa sumu kali wakati wa kampeni za uchaguzi lakini hatukuweza kubaini ni nani alifanya hivyo lakini tulijua ni mambo ya siasa na nikamwachia Mungu.

Katika hatua nyingine Mr Nice alisema Tanzania kuwa na wasanii wengi kwenye tuzo za MTV MAMA 2016 kuliko jirani zake Kenya na Uganda kulitokana juhudi za msanii moja moja.

“Kusema kweli wasanii wa Tanzania wamekuwa wakishindana wenyewe kwa wenyewe, kila mmoja anataka kufanya kazi nzuri kuliko mwenzake. Kwahiyo binafsi naona hii hali imesaidia kuwajenga wasanii wa Tanzania pamoja na muziki kiujumla,”
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. kuna picha katika mtandao ilionyesha kweli Mr Nice alikuwa amekonda sana ndiyo sababu watu wanafikiri ana ukimwi na ndiyo maana haoatti kazi bongo mpaka aende nchini kenya, lakini watanzania acheni ubaguzi hata kama mtu akiwa na ukimwi ni mtu wakawaida kama wote

    ReplyDelete
  2. Ukimwi unajulikana kwa kupimwa,ungemwambia hivyo mwandishi uende nae kwenye kituo cha afya ukapimwe.fyuuuuuu

    ReplyDelete
  3. Ukimwi sio ugonjwa wa rahana, ukimwi ni ugonjwa kama magonjwa mengine, watu wengi mna ukimwi ila hamjijuhi. Utasikia watu wengi tena mastaa wanajigamba na kuonyesaha vyeti vyao kuwa oho angalia cheti changu kinaonyesha sina ikimwi!!! Ukitaka vipimo vya huakika njoo ukapimwe huku USA utashanga na utafunga mdomo wako.

    ReplyDelete
  4. kwani ni lazima aende kupima kwani wao waandishi wamepimwa si ajabu na waandishi wanao

    ReplyDelete

Top Post Ad