Trey Songz Amenipa 'Kiki' Hadi Marekani - Vanessa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Msanii wa muziki wa bongo fleva, mwanadada Vanesa Mdee a.k.a Vee Money, amefunguka na kueleza faida alizopata kwa kuwa karibu na nyota wa muziki nchini Marekani Trey Songz.

Akiwa katika kipindi cha FNL cha EATV, Vanessa alitakiwa kueleza faida alizopata kutokana na skendo zilizovuma siku za hivi karibuni kuwa alitoka kimapenzi na Trey Songz kipindi walipokuwa nchini Kenya katika Coke Studio.

Katika majibu yake, Vanessa alisema kuwa hakuna jambo linalovuma kwake bila ya kuwa na faida, na kwamba skendo hizo zilivuma hadi Marekani, kwani aliandikwa katika baadhi ya blogs za Marekani kuhusu ukaribu wake na Trey Songz, kitu kilichomfanya kujulikana hadi katika taifa hilo lenye nguvu katika karibu kila nyanja, ikiwemo muziki duniani.

Katika FNL ya Sam Misago ilikuwa hivi.......
Swali: "Vipi ishu ya wewe na Trey Songz imekupa faida gani, je kuna Wamarekani wamekujua au imeishia hapa hapa?"

Jibu: "Yea, hakuna jambo naweza fanya bila manufaa, hiyo imenifanya niandikwe kwenye blogs kadhaa nchini Marekani, kwahiyo wamarekani wamenijua"

Trey Songz amekuwa akifananishwa kimuonekano na mpenzi wa Vanessa, Jux licha ya Jux mwenye kuweka wazi kuwa Trey Songz ndiye role model wake.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wananchi gani wamekujua mpumbavu wewe. Kumbe ndivyo mnavyokaaa na kujidanganya. Hivi Raia wa Marekani ni kweli wanaweza kuacha shughuli zao na kuanza kutaka kujua hako ka Vanessa ni nani. Kwa kweeeeliiiii ulimbukeni ni kitu kibaya sana. Mkiambiwa nendeni shule mkafute matongotongo yenu hamtaki kusikia. Sasa angalia huyo mwanamuziki uchuro anachokizungumza. Ni uchwara mtupu........... Kujulikana ujulikane umekuwa nani weweeeeeeeeee......

    ReplyDelete
  2. Hahhahhahahahha mdau amekukwaza eeeh....huyu bint naona andiko lako si la kawaida ni povu la mwendokasi....

    ReplyDelete
  3. mimi naishi marekani na sijaona blogg yeyote iliyoandikwa kuhusu Vanesa na mimi ni msomaji sana wa blogg

    ReplyDelete

Top Post Ad