MANJI Asalimu Amri...Aanza Kuamisha Kampuni zake Kutoka Jengo la Quality Plaza

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wapangaji katika jengo la Quality Plaza lililopo barabara ya Nyerere jijini Dsm wametekeleza Amri ya Mahakama kuu kitengo cha ardhi cha Kuondoka katika jengo hilo baada ya kutolewa saa 24 ambazo zimemalizika asubuhi ya leo,huku kampuni ya Yono ikisimamia zoezi hilo lililoendeshwa Chini ya Ulinzi mkali .

Majira ya Saa mbili Asubuhi Channel ten imeshuhudia wapangaji katika jengo hilo wakihamisha samani zao,huku ikielezwa kuwa makampuni zaidi ya matano yaliyopangishwa chini ya Kampuni mama ya Quality Group ilianza kuondoa mali zao usiku wa kuamkia leo.

Mkurugenzi wa Yono ambayo imepewa Kibali cha kuwahamisha wapangaji hao na Mfuko wa hifadhi ya jamii -PSPF amesema jengo hilo hivi sasa liko chini ya Usimamizi wao mpaka pale wapangaji wote watakapondoka. w

Dalali wa Mahakama kuu kitengo cha Ardhi Yono Steven Kevela amesema zoezi hilo la kuwahamisha wapangaji sugu wasiolipa pango na kukamata mali zao na kuzipiga mnada litaendelea kwa kasi na kuwataka wote waliopewa notisi za kulipa katika kipindi cha Siku saba kutekeleza kinyume chake sheria itachukua Mkondo wake.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. CCM fyu
    Wizara za serikali zimo mbona hamwafukuzi wizara ya afya idaiwe bilion eti walipe 300000

    ReplyDelete

Top Post Ad