MCHEZAJI Yaya Toure Ashtakiwa Kwa Kuendesha Gari Akiwa Amelewa...Mwenyewe Adai Yeye ni Mwislam

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mchezaji wa klabu ya Manchester City ambaye ni raia wa Ivory Coast Yaya Toure amesema hajapinga shtaka la kuendesha gari akiwa amelewa wiki mbili zilizopita.

Hata hivyo, amesema kwamba hakunywa pombe makusudi alipokamatwa akiendesha gari akiwa mlevi.

Ameandika kwenye Facebook kwamba “inafahamika wazi kwamba mimi ni Mwislamu na huwa sinywi pombe.”

Hata hivyo, hajaelewa ni vipi alijipata akinywa pombe ama akajipata akiwa amelewa bila yeye kufahamu.

Gazeti la The Mirror la Uingereza linasema kwamba alidai alikunywa Diet Coke na hakujua kwamba kwenye jagi aliyokuwa akitumia kunywa palikuwa pameongezwa kilevi aina ya brandi.

Gazeti hilo linasema amepigwa marufuku kutoendesha gari kwa miezi 18 na kupigwa faini ya $68,000 (£54,000).

Mchezaji huyo amesema: “Daima nimekuwa nikikataa pombe. Yeyote anayenifahamu na anayefuatilia uchezaji wangu atakuwa bila shaka ameniona nikikataa shampeni ya Mchezaji Bora wa Mechi kwa sababu ya kujitolea kwangu kuheshimu dini yangu.”

“Ni muhimu kwangu kwamba niliiambia mahakama kwamba sikunywa pombe makusudi. Jaji akinihukumu mwenye alikubali kwamba sikuwa nimekunywa pombe makusudi.”

Amesema kesi yake ilihitimishwa Jumatatu na kwamba alikubali shtaka.

“Kuendesha gari ukiwa mlevi ni kosa kubwa na ingawa sikunywa pombe makusudi, nakubali marufuku na faini na naomba radhi kwa yaliyotokea,” aliongeza.

Source: BBC
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. HA HA HA HA HA ETI MWISLAMU HANYWI POMBE!!!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Si eti ni haramu kabisa kwa mwislamu kunywa pombe kabisa kilevi chochote mtu akifanya ni jeuri yake tu na nithambi I hop umenielewa.adding more pia nyimbo ni haramu hao wanao imba wanafanya bt ukweli unabaki ukwali daima

      Delete
    2. Si eti ni haramu kabisa kwa mwislamu kunywa pombe kabisa kilevi chochote mtu akifanya ni jeuri yake tu na nithambi I hop umenielewa.adding more pia nyimbo ni haramu hao wanao imba wanafanya bt ukweli unabaki ukwali daima

      Delete
  2. pia walevi wengi huwa wanajificha kuwa hawanywi pombe, lakini wakiwa peke Yao majumbani kwao wanakunywa balaa yaani ni moto wa kuotea mbali nasemea kwa huku majuu ulaya

    ReplyDelete

Top Post Ad