TAARIFA ya Kusikitisha Kutoka Kata ya Masanze Jimbo la Mikumi.

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

OFISI YA MBUNGE Jimbo La Mikumi inalaani sana kitendo cha kinyama kilichofanywa na Ndugu zetu wa jamii ya wafugaji kwa kujichukulia sheria mkononi na kumjeruhi vibaya Ndugu Augustino Mtitu mkulima wa kitongoji cha Upangwani, Kijiji cha Dodoma Isanga, Kata Ya Masanze Jimbo la Mikumi ambapo leo tarehe 25 Desemba majira ya Mchana amechomwa mkuki mdomoni na kutokezea nyuma ya shingo yake, ambapo alipelekwa hospitali ya wilayani Kilosa na baadae amekimbizwa hospitali ya mkoa Morogoro  ili kufanyiwa operesheni ya kuondoa mkuki huo na kwa matibabu zaidi.

Augustino Mtitu alishambuliwa na wafugaji wa kimasai alipokuwa akimsaidia jirani yake kufukuza Ng'ombe wasiharibu mazao shambani kwake, Kipande cha mti kinachoonekana hapo mdomoni ndiyo mkuki uliokatwa ili kupunguza urefu wa mkuki huo wakati wakimkimbiza hospitali,  Inasemekana MwenyeKiti wa kijiji na MwenyeKiti wa kitongoji hicho nao wamejeruhiwa.

WITO KWA SERIKALI.
Ofisi Ya Mbunge Mikumi inatoa wito kwa Serikali  kuwabaini wale wote waliofanya kitendo hiki cha kinyama kuhakikisha wanachukuliwa hatua kali za kisheria  ili kuweza kukomesha vitendo hivi vya kujichukulia sheria mkononi inayopelekea kuongezeka kwa uvunjifu mkubwa wa Amani na migogoro isiyokwisha kati ya wakulima na wafugaji wilayani KILOSA.

Imetolewa na:-
Robert A. Galamona
Katibu Ofisi Ya Mbunge
Mikumi.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Unyama wa hali kubwa. Lini Serikali yetu itachukua majukumu kuondoa tatizo hili. Ni elimu tu inatakiwa hapa. Usalama wa raia ni kitu kikubwa sana. Angefanyiwa mtalii, mzungu Serikali ingehangaika kumchukulia ndege sababu ingebanwa. Kwa nini WAtanzania tunakubali na kuwa kimya mwenzetu anapovamiwa. Kwa nini tusiishike serikali kutujali. Elimu kwa wananchi kuhusu kuua, kupora, kutumia mapanga. Hii inabidi mhusika anyongwe mara moja ili watu waishi kwa amani. Sheria zinawabana wasio na hatia, wenye hatia hawachukuliwi sheria vipasavyo. Hii ni aibu kwa nchi na inabidi uongozi ujitafakari. Mtanzania hana Thamani mpaka awe tajiri au kiongozi wa siasa au ndugu zao?Lini tutajithamini wenyewe.

    ReplyDelete

Top Post Ad