BOSI Ndege za Serikali Afariki

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


OFISA Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA), Kapteni Keenan Mhaiki, amefariki dunia jana saa 5:25 asubuhi katika Hospitali ya Agha Khan Jijini Dar es Salaam.

Alilazwa katika hospitali hiyo Alhamisi iliyopita, kabla ya sikukuu ya Krismasi, kwa ugonjwa wa saratani ya ini.

Kaka mkubwa wa marehemu, ambaye aliwahi kuwa Katibu Mkuu katika Wizara ya Sheria, Oliver Mhaiki alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na HabariLeo.

Mhaiki alisema Kapteni Keenan ambaye ameendesha marais wa awamu zote tano, alianza kuumwa Julai mwaka huu kwa kusumbuliwa na pingili ya ‘lumber’, hali iliyoelezwa na madaktari ni kwa sababu ya kukaa muda mrefu.

Alisema marehemu alikuwa akisumbuliwa na maumivu na Oktoba mwaka jana alipokwenda India kwa ajili ya uchunguzi zaidi, ndipo baadaye alirudi kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji.

“Kilichomuua sio hicho, inaonekana alikuwa na saratani ya ini muda mrefu, hakuigundua, hivyo wiki mbili zilizopita alibadilika rangi kuwa njano, alipoenda hospitali wakagundua ni saratani,” alisema kaka huyo wa marehemu.

Alisema marehemu ameacha mke na watoto wawili na kwamba anatarajiwa kuzikwa Songea. Alisema hivi sasa wanasubiri wadogo wa marehemu waliopo nje ya nchi.

Alisema katika familia yao, wamezaliwa watoto nane.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Saratani ya ini ugonjwa huo unaitwa Hepatit C ukiwahi kutibiwa mapema utapona lakini ukikaa nao kwa muda mrefu niyo mtu unaugua na kuwa manjano na mwishowe hufariki. R.I.P

    ReplyDelete

Top Post Ad