Mwili wa Mwanafunzi Waopolewa Ziwani

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mwili wa mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Sekondari ya Chato mkoani Geita, Shilinde Nicolaus (18) umeopolewa Ziwa Victoria baada ya kuzama Januari 28 saa tisa alasiri alipokuwa akivua na wenzake.

Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Mponjoli Mwabulambo alisema  mwili huo ulipatikana juzi baada ya jitihada za wavuvi wa eneo hilo kwa kushirikiana na wananchi.

Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Muungano lilipotokea tukio hilo, Kapembe Charles alisema kijana huyo na wenzake ambao walinusurika, walipata ajali hiyo  baada ya mtumbwi wao kupigwa na dhoruba kisha kuzama.

Charles alisema katika tukio hilo wenzake wawili, Daud Deus na Mgonyolo Hamis wote wakazi wa Kijiji cha Kitela walinusurika  baada ya kuogelea hadi nchi kavu.

Mmoja wa wanafunzi hao, Daud Deus alisema wakati wakiendelea  kuvua, kulikuwa na upepo mkali uliosababisha mtumbwi wao kuzama.

“Mimi na Hamis tulifanikiwa kuogelea kwenye majani yaliyoota ndani ya maji, kisha tukaokolewa na wavuvi,” alisema Deus.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad