Prof Lipumba Anusurika Kipigo Kutoka kwa Vijana wa Ukawa, Akimbilia Msikitini Kujinusuru..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


MWENYEKITI wa Chama Cha Wananchi (CUF) anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba amenusurika kupigwa na vijana wanaoaminika kuwa ni wa Ukawa wakati akitoka kwenye mkutano wa kampeni mjini Morogoro.

Katika vurugu zilizotokea juzi jioni wakati vijana wa Ukawa na kikundi cha ulinzi cha CUF (blue guard) cha Dar es Salaam wakiwa na Profesa Lipumba walikuwa wakitoka kwenye mikutano ya kampeni maeneo tofauti walipokutana barabarani na kuanza kurushiana maneno na hatimaye kupigana.

Katika vurugu hizo, vijana wa Ukawa waliwazidi wenzao wa blue guard na Profesa Lipumba kulazimika kukimbilia kwenye Msikiti wa Mungu Mmoja Dini Moja ili kujinusuru.

Ghasia hizo zilizodumu kwa takribani saa moja na nusu ambapo baada ya Profesa Lipumba kukimbilia msikitini hapo, wafuasi wa Ukawa walibaki nje mpaka polisi walipofika na kuwatawanya.

Akizungumzia tukio hilo, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonce Rwegasira alikiri kutokea kwa vurugu hizo ambapo alisema wafuasi watatu wa CUF walijeruhiwa.

Alisema kuwa polisi wanaendelea na uchunguzi ili kuwabaini walioanzisha vurugu hizo ikiwa ni pamoja na kuweka doria kali katika mikutano ya vyama vya siasa.

Profesa Lipumba hakupatikana jana kuzungumzia suala hilo, baada ya simu yake kutokuwa hewani jana.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. mmmh tunatoana roho yarabiii kwa mali alizoacha baba mali ya baba inatutoa roho bora nikae pemeni niinusuru rohoyangu mimi

    ReplyDelete

Top Post Ad