Hana Hamu ya Kufanya Mapenzi na Mimi..Naomba Ushauri

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 30, nina mpenzi wangu wa muda mrefu toka 2014 japo mapenzi yetu yamekuwa hayana muendelezo muzuri kutokana na tabia za huyu mwenzangu. Tulianza mahusiano yetu vizuri sana baadae mwenzangu alibadilika ghafla, nikaja kugundua alikuwa na mahusiano na wanaume wengine (zaidi ya mmoja) tukawa tumepotezana kwa mda kidogo coz alikuwa hapokei simu wala kujib text zangu alafu akawa ni mtu wa kusafiri sana kumbe alikuwa anasafiri na hao mabwana zake, siku nimekutana nae nilimuona na dalili za mimba roho iliniuma sana, mwanzoni alidanganya baadae akakubali akawa ametoa hiyo mimba akaomaba nimsamehe kwa sababu nampenda sana tena sana nikawa nmemsamehe. 

Tukawa pamoja kwa mda mfupi baadae alianza tabia yake ya kuruka ruka na starehe kwa sana, niliamua kumuacha japo roho ilikuwa inaniuma alafu yeye hata hajali kila kitu kwake poa tu. Baadae alirudi akaanza kunitafuta akaomba msamaha kama kawaida yake, kupenda ni hatari sana jamani nilimsamehe tukaanza kuwa pamoja, alikaa kwangu kwa muda wa week, nikaanza michakato kwenda kutoa posa na mahari kwao.

Sasa alivyorudi nyumbani kwao akaanza tena unaweza mpgia simu anakuambia sipo nyumbani nipo kwa dada angu fulani, au kwa bibi nitarudi kesho, au nipo hospitali bibi anaumwa baadae simu inapotea hewani hata siku mbili akipatika anakuambia huku kijijini simu ilizima charge. Sasa kilichonichosha zaidi sasahivi hana hata hamu ya mapenzi kabisa tofauti na navyomjua mimi, huyu mpenzi wangu hapo awali alikuwa akiniona tu hutumii nguvu nyingi kumuandaa, lakini sasa hivi hata ukifanyeje hawezi kuwa tiyari hadi umpake mafuta kidogo. na unaweza kumuomba hata mwezi nzima anakuambia sijisikii, sina hamu.

Naomba ushauri wadau, nifanje ili aweze thamini hisia zangu, au hata kama nikimuacha nifanyeje coz nampenda sana huyu dada natamani awe mke wangu wa ndoa, kuna vitu huwa vinanifanya nimpende sana ni rafiki, mnataniana na kucheka, mpole ila sasa ndo hayo mambo yake, nilishajaribu kumuacha nashindwa nafuta namba kila kitu ila akinipigia tu au nikumuona tu nabadilisha mawazo.

By Von G
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Replies
    1. Kuhusu habari za mapenzi, kuna mwanafalsafa mmoja alsema hivi. UKIPENDA SANA, UKIJA KUACHA UTAUMIA SANA. KWA HIYO PENDA WASITANI ILI UKIJA ACHWA UTAUMIA WASTANI. KUWA NA MSIMAMO. MWANAMKE UNATAKIWA UMPENDE WASTANI. Hata kama utampenda usioneshe dhahiri kuwa unampenda. Angalia yote hayo yanavyokutesa. Piga moyo konde, achana naye kwani wanawake ni wengi kuliko unavyozani tena wazuri kuliko huyo uliyenaye. Anakufanyanyia hivto wakati mko kwenye uchumba tuu jee mkioana itakuweje? si utajinyonga wewe kama wenzetu wa mkoa Fulani wa nyanda za juu kusini!!!!!!!!!!!!!

      Delete
    2. upuuzi mtupu

      Delete
  2. tatizo liko kichwani mwako. kumbuka huyo siyo mke wako, ni mpenzi tu. na hilo swala la kufanya mapenzi kabla ya ndoa ni makosa na ni dhambi kwa Mungu. Achana naye na umfute kabisa akilini mwako. usiwe limbukeni wa mapenzi. huyo dada hakupendi ila wewe ndo unajipendekeza na unaonesha kabisa kuwa unamnyenyekea sana!!!! hata ukijitahidi ukamwoa, atakuja akutese na utajuta! ni mara mia kuvunja hayo mahusiano kuliko kuja kuvunja ndoa na kuwafanya watoto wakose malezi bora ya wazazi huku wote mkiwa hai!achana naye kabisa na umsahau kabisa. wapo wanawake wengi wazuri kuliko hata huyo na utampata anayeendana na wewe. kama unamcha Mungu mwombe akusaidie kupata mchumba sahihi. kama hakuthamini kabla ya kuishi naye kamwe hatakuthamini mkiishi pamoja. achana naye kabisa HAKUPENDI ACHA KULAZIMISHA MAPENZI!!!!!

    ReplyDelete
  3. Baada ya mkutia yeye hicho kilainisho hukutueleza ikiwa na wewe pia unajitia.

    ReplyDelete
  4. Huyo mwanamke hakufai kabissa achana nae atakuletea maradhi na utakufa ukiwa ujaiona na ukigundua yeye ndiye chanzo cha kuumwa kwako unaweza fanya kitu kibaya sana. Ingekuwa umezaa nae basi ungevumilia hili mlee watoto, lakini kama hakuna commitment yoyote basi achana nae utapata mwingine na utampenda na yeye atakupenda, huyo mwanamke hakupendi na ndiyo maana ana-cheat, na ku-cheat kwa mwanamke yeyeyote mwenye commitment ni dharau kubwa kwa mwenza wake ni uadui mbaya kuliko kitu chochote. Kwa kifupi huyo mwanamke siyo mpenzi wako ila ni adui yako mkubwa na hakufai kabisa achana nae hyu siyi ndugu yako bali ni rafiki yako tu mmekutana njiani huyo ana pepo mbaya wa ngono kitu ambacho kwako kitakusabishia umauti lakini kabla utapata mateso sana. Hao mwalimu wao ni kipofu.

    ReplyDelete
  5. Tatizo unakuwa na nyodo, mzembe kitandani na unataka ufanyiwe mahaba wewe tu bila kumfanyia na mwenzio. Mbaya zaidi hauna ubunifu wowote upo tu kama sanamu kisa wewe ni mzuri na unavutia unasahau kuwa ladha ileile kilasiku inachosha. Nyama choma, supu, mishikaki, na rosti ni kwaajiri ya radha tu lakini nyama ni ileile.
    NASEMA BADILIKA!

    ReplyDelete
  6. wewe hujajua kaka...hicho kilainishi anataka ule kisamvu...mwenzio washamuanzishia mchezo huo we hujui jarbu kugusa samvu uone kama atachomoa

    ReplyDelete

Top Post Ad