Hii Ni Zaidi ya Kazi Kazi..Vita Madawa ya Kulevya Vyageukia Makaniani,Wachungaji Sasa Kubeba Mzigo Huu..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato mkoani Mara, George Ojwang’ amewaagiza wachungaji na wazee wa kanisa hilo kuwashughulikia waumini wao wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

Aliyasema hayo katika sherehe za kumsimika mchungaji mpya wa Mtaa wa Mauwe ulioko Kitembe Rorya.  Alisema kama kanisa litakuwa safi, Serikali haitakuwa na muda wa kushughulikia watu kama hao wanaosababisha kupotea kwa nguvu kazi ya Taifa.

Katika tukio jingine, Mkoa wa Tabora umezindua kampeni ya kupambana na dawa za kulevya na wahusika wakionywa kutofanya mzaha katika vita hiyo.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita mjini hapa, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri alisema tayari kamati zote za ulinzi na usalama za wilaya zimepewa maelekezo ya kufanya.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Hamis Issa alisema kati ya Februari 13 na 16 wamekamata dawa za kulevya mbalimbali zikiwamo cocaine, mirungi, bangi na mbegu zake.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad