Kocha Msaidizi Amtaja Aliyeiangusha Yanga

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mara baada ya Yanga kuchezea kipigo cha mabao 2- kutoka kwa mahasimu wao Simb, Kocha Msaidizi wa Yanga Juma Mwambusi amefunguka sababu za timu yake kupoteza mchezo mojawapo ikiwa ni kuumia kwa kiungo wake Thaban Kamusoko.

Mwambusi amesema kuumia kwa Kamusoko kuliwafanya Simba waje zaidi katika eneo la katikati, jambo ambalo liliwasaidia kupitisha mipira kirahisi na hatimaye kuweza kupata mabao mawili na kuibuka na ushindi.

Amesema licha ya kumuigiza Said Makapu kuchukua nafasi ya Kamusoko, lakini hakufanya kazi ipasavyo, na pia anapungukiwa baadhi ya vitu alivyonavyo Kamusoko ikiwa ni pamoja na kuwa na maono pamoja na kuunganisha safu ya nyuma na mbele.

Sababu nyingine aliyoitaja Mwambusi ni umakini wa wachezaji wote kwenye timu yake kupungua na kushindwa kukaba, jambo lililofanya wawe wanakaba kwa macho.

"Wao Simba waliongeza namba katikati, sasa na sisi vijana wetu tuliowaingiza baada ya kamusoko kuumia walipaswa walitakiwa kuongeza namba katikati lakini wakashindwa,.... Pia umakini wa ukabaji kwa wachezaji wetu haukuwa mzuri, Simba walikuwa wanakuja wanapita watu wanawasindikiza kwa macho" - Amesema Juma Mwambusi.

Hata hivyo amesema matokeo hayo inagawa yanawaumiza, hayajawapotezea lengo lao la kutwaa ubingwa wa ligi kuu Tanzania na kwamba atakaa na walimu wenzake kurekebisha makosa ambayo yamejitokeza ili yasijirudie tena.

Katika mchezo huo, mabao ya Simba yalifungwa na Mavugo na Kichuya kipindi cha pili, huku la Yanga likifungwa na Msuva kwa njia ya penati, katika dakika ya 5
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mimi ni Azam,kufungwa kwa yanga ni moja kati ya matokeo,kushinda/kushindwa/sare.
    kushindwa ni lazima kuwe na sababu,yeye katoa sababu na
    hata wangekuwa simba wangetoa sababu.
    Sioni kama Simba ni wazuri sana kuliko yanga,baada ya kamusoko kuumia kama simba wangekuwa wazuri sana kwa nini wasingewafunga 4......?Ila kwa simba kumfunga yanga ndio sherehe yenyewe tofauti na azam alivyowafunga YANGA na SIMBA.
    Wakati mwingine ni bahati tu.

    ReplyDelete
  2. Ni arosto bana ndio ilowasumbua

    ReplyDelete

Top Post Ad