MREMA Aibuka Sakata la Madawa ya Kulevya..Ampinga Lissu Kutetea Watuhumiwa wa Dawa Hizo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


MWENYEKITI wa Parole, Augustino Mrema amemshukia Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), kuwa anafanya makosa makubwa kutetea watuhumiwa wa dawa za kulevya.

Akizunguma na MTANZANIA kwa simu jana, Mrema alisema anamshangaa Lissu kuwatetea watu wanaojihusisha na dawa za kulevya na kumshauri atumie elimu yake ya sheria kuwatetea waathirika na wanaotaja wahusika wa dawa za kulevya akiwamo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Mbali na Lissu, Mrema aliigeukia  mahakama itambue kuwa pamoja na kutafsiri sheria, jukumu la kuzuia dawa za kulevya lipo mikononi mwao.

“Nashangazwa na hawa wanaotuhumiwa kukataa kwenda kupimwa na kuonyesha juhudi za kuzuia zoezi hilo, wakubali kwenda kupimwa kwani ndio itakuwa kusafishwa kwao kama majibu yatatoka kuwa hawatumii,” alisema Mrema.

Akizungumzia kauli hiyo, Lissu alisema Mrema anapaswa kujiuzulu cheo alichopewa cha Mwenyekiti wa Parole kwa sababu alipewa kinyume cha sheria.

Alisema sheria ipo wazi kwamba Mwenyekiti wa Parole awe jaji au alishawahi kuwa jaji na si mwanasiasa kama Mrema.

“Ninapoona Mrema anapiga kelele, anatetea chakula chake na si vinginevyo, kisheria Mwenyekiti wa Palore anapaswa kuwa jaji au alishawahi kuwa jaji,”alisema Lissu.

Aidha kuhusu kuwatetea watuhumiwa, Lissu ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Chadema, alisema sheria ipo wazi kwamba                                                                                                                                                                                                                       wanachofanya mawakili kwa sasa ni kuwatetea watuhumiwa wote hata wanaotuhumiwa na dawa za kulevya, kwani sheria inamtaka wakili kutetea yeyote bila ubaguzi.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mwizi humtetea mwizi mwenzie.

    ReplyDelete
  2. MTU ALIYEUWA ANATETEWA SEMBUSE WA MADAWA YA KULEVYA!!!!!!

    ReplyDelete
  3. Bwana Mrema nakuunga mkono kwa kauli moja hili baa la madawa ya kulevya ni janga la taifa lakini Kina lisu watakula wapi wakiona aibu kutetea wahalifu kila leo wanawaombea watu watende uhalifu kwa sababu wakiwatetea ndo shibe yao laa sivyo bila kesi kina Lisu njaa zitawaua siunawaona midomo ka kasuku hii ni ajira yao wengine wanatoka jasho kujipatia riziki

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kina Lissu wanajua kupiga pesa tuu huku vijana wanateketea

      Delete

Top Post Ad