Paul Makonda Aeleza Kilichomfanya Kutaja Majina ya Watuhumiwa wa Madawa ya Kulevya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa uamuzi wa kuwataja hadharani majina ya watuhumiwa wa biashara ya dawa za kulevya ni kutokana na maombi ya Watanzania waliyayotoa wakati wa serikali ya awamu ya nne.

Makonda alisema kuwa licha ya watu wengi kupaza sauti zao wakitaka watuhumiwa wa dawa za kulevya watajwe hadharani, lakini Rais Mstaafu, Dkt Jakaya Kikwete yeye hakuwataja huku akiacha vyombo husika vifanyekazi zao kwa usiri.

Lakini kwa upande wa serikali ya awamu ya tano, waliamua kuwataja watuhumiwa hao ikiwa ni kujibu maombi ya kile watanzania walichokitaka tangu kipindi cha nyuma, alisema Makonda jana akiwa kwenye semina ya Walimu Wanaosomesha Quran Tanzania (JUWAQUTA).

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza katika unafunguzi semina ya Walimu wanaosomesha Qur-an Tanzania (JUWAQUTA) leo jijini Dar es Salaam.

“Mzee Jakaya mlimpigia kelele taja, taja, taja, taja, sasa tulipoingia sisi tukaona wacha tufanye kama alivyokuwa mnataka” alisema RC Makonda.

Aidha, RC Makonda amewakosoa wote walioibuka na kumdhihaki sababu alitaja majina hayo akisema kuwa giza haliwezi kuondolewa kwa giza bali ni kuwaleta waliopo gizani kwenye nuru.

“Uliona wapi giza linaondolewa kwa kutumia giza? Aliyefanya mafichoni anawekwa hadharani na harudii tena,” alisema Makonda.

Katika awamu ya tatu ya vita dhidi ya dawa za kulevya, RC Makonda hakutangaza majina hadharani kama alivyofanya katika awamu mbili zilizopita ambapo alimkabidhi majina 97, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya Rogers Sianga ili ayashughulikie.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. you dont have excuse what you did is very wrong ni kweli tunapinga vikali madawa but ungetenda haki kwa wote isitoshe magwiji wenyewe mbona hukuwataja? na wanajulikana tumepata picha safi kumbe mukitongoza na mukikataliwa after munalipiza kwa kuwadhalilisha watu enough makonda dont talk too much tumekutambua

    ReplyDelete
  2. Watu Waliingojea List ya Raisi Kikwete . Walidai ndiyo sababu alishindwa kuitaja na kuwachukulia watu hatua. Hii iliwafanya watu wamwambie aitaje akashindwa kuitaja.
    Leo mnawaonea wavutaji, MMewaachia vigogo na watoto zao wenye uwezo wa kuingiza bila kushikwa. Wao ndio Watanzania wanataka muwataje.

    ReplyDelete
  3. Makonda tunakuombea sana,kwa kweli kwenye hili la madawa ya kulevya ninachoamini litaishia hewani kwa kuwa vigogo wengi wanatetea na kukuvunja nguvu.

    ReplyDelete

Top Post Ad