Baada ya Kuachiwa Huru..Nay wa Mitego Aaalikwa Ikulu Kuteta na Rais Magufuli..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Msanii wa muziki wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki maarufu kama Nay wa Mitego ameitwa Ikulu jana jioni  kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Rais John Magufuli.

Nay alipata mwaliko huo ikiwa ni sasa chache baada ya kuachiwa huru na Jeshi la Polisi lililokuwa likimshikilia tangu juzi.

Katika mahojiano yake na kituo cha Televisheni cha Azam Two,  Nay alikiri kupata mwaliko huo na kueleza kuwa ataitumia vyema nafasi hiyo kumuelezea Rais Magufuli hali halisi ya maisha ya Watanzania.

“Nimepokea mwaliko bado nafikiria nini cha kuongea naye endapo nitapata hiyo nafasi ya kuzungumza naye, nadhani itakuwa nafasi nzuri ya kumweleza vile ambavyo Watanzania sisi tunaishi mtaani,”alisema.

Nay alikamatwa na polisi juzi mkoani Morogoro na kusafirishwa hadi Dar es Salaam kwa kile kilichodaiwa kutunga wimbo wenye maudhui yanayoikashifu Serikali.

Mapema jana mjini Dodoma, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe alisema Rais Magufuli ameagiza msanii huyo aachiwe huru na wimbo wake uendelee kuchezwa na kusambazwa.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad