CCM Yaibwagia TOT ‘Zigo’ Madai ya Mke wa Komba..!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimemtaka Salome Komba ambaye ni mke wa kada maarufu wa chama hicho, marehemu Kapteni John Komba, kufuatilia malipo ya mafao ya mumewe kwa uongozi wa kundi la Tanzania One Theatre (TOT) ambako ndiko alikokuwa akifanyia kazi.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Rodrick Mpogolo, ametoa maelekezo hayo ikiwa ni siku moja tu baada ya Salome kukaririwa  akimuomba Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli aingilie kati kumsaidia ili alipwe mafao ya marehemu mume wake yanayofikia Sh. milioni 75.

Kwa mujibu wa Salome, hadi sasa wakati mumewe akitimiza miaka miwili tangu afariki dunia, CCM imemlipa Sh. milioni 4.5 tu ikiwa ni sehemu ya malipo hayo huku akifuatilia kwa muda mrefu bila mafanikio kupata kiasi kilichobaki cha Sh. milioni 70.5.

Akizungumza  jana kuhusiana na suala hilo, Mpogolo alisema ofisi yao haiwezi kulizungumzia kwa sababu masuala yanayohusu fedha yanapaswa kufafanuliwa vyema na uongozi wa kundi lao la TOT ambako Komba alikuwa akifanya kazi.

“Ukiniuliza mimi chama kinasemaje (kuhusiana na madai ya mke wa Komba), sidhani kama nitaweza kuzungumzia hilo kwa kuwa ni suala la fedha … na masuala ya fedha si unajua… yana taratibu zake za kifedha. Aulizwe Mkurugenzi wa TOT anaweza kusema nini kinaendelea,”alisema Mpogolo.

Jitihada za  kumpata Kaimu Mkurugenzi wa TOT, Gasper Tumaini, ili azungumzie suala hilo hazikufanikiwa jana. Hata hivyo, Tumaini alikaririwa pia jana akionyesha kufahamu deni hilo.

Komba aliyezaliwa mwaka 1954, alifariki dunia Februari 28, 2015 na kuzikwa mkoani kwake, Ruvuma. Enzi za uhai wake, Komba alijizolea umaarufu mkubwa kutokana na umahiri wake katika kutunga na kuimba nyimbo mbalimbali za kwaya, hasa za kukipigia debe chama chake (CCM) wakati wa kampeni za uchaguzi.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad