Hatarii...Aliyekuwa Waziri wa Kikwete Sasa Aisoma Namba,Ashindwa Kulipa Deni la Milioni 11,Alilia Asamehewe...!!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Katika hali inayoonyesha hali ngumu ya kiuchumi, aliyekuwa Naibu Waziri wa Kazi na Ajira na Maendeleo ya Vijana, katika Serikali ya Awamu ya Nne, Makongoro Mahanga ameamua kujisalimisha na kumwangukia Kainerugaba Msemakweli ili amsamehe deni analomdai.

Hata hivyo Msemakweli amesema hawezi kumsamehe Mahanga kutokana na kwamba ameshatumia gharama katika kesi yake hivyo lazima alipwe fedha zake.

Mahanga anatakiwa kumlipa Msemakweli jumla ya Sh11, 097,000 na anatakiwa kulipa Sh2 milioni kila mwezi kwenye akaunti ya

Msemakweli na kisha kuwasilisha mahakamani risiti ya malipo, hadi deni hilo litakapomalizika.

Deni hilo ni gharama za kesi alizozitumia Msemakweli katika kesi ya madai ya kashfa iliyofunguliwa na Mahanga dhidi yake baada ya kumtaja katika kitabu chake cha Orodha ya Mafisadi Sugu wa Elimu kuwa ni mmoja wa vigogo wenye shahada za Udaktari wa Falsafa za kughushi.






----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad