JPM: Serikali Haitatoa Chakula Bure kwa Wenye Njaa..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameendelea kusisitiza kuwa kuwa Serikali haitatoa chakula cha msaada kwa watakaopatwa na njaa ilihali wanaweza kuzalisha chakula katika maeneo yao.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo jana katika ziara yake mkoani Pwani, wakati akizungumza na wananchi wa Somanga, Nangurukuru na Mchinga Moja, ikiwa ni ziara yake katika mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara.

Amepokea kero za wananchi katika maeneo hayo na kufanya kazi kwa bidii ikiwemo kuzalisha mazao ya chakula cha kutosha

"Najua mmezoea kusikia maneno mazuri mazuri kuwa hakuna atakayekufa kwa njaa, sasa mimi nasema usipofanya kazi, usipolima mazao na kupata chakula wakati mvua inanyesha Serikali haitatoa chakula cha bure kwa wenye njaa, ni lazima tufanye kazi, sasa hivi mvua zinanyesha limeni mazao ya chakula" amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.

Pia Rais Magufuli amezungumza na wananchi wa Ikwiriri na kupokea kero zao ambapo amewaagiza Mamlaka ya Maji katika Mji huo kuhakikisha mradi wa maji uliojengwa na kukamilika tangu mwaka 2015 kwa gharama ya Shilingi Bilioni 5, unaanza kutoka maji kabla ya mwisho wa Mwezi huu na pia amepiga marufuku utozaji wa ushuru kwa wafanyabiashara wadogowadogo wa mazao.

Aidha, Mhe. Dkt. Magufuli amewaagiza viongozi wa Mkoa wa Lindi kushughulikia migogoro ya wakulima na wafugaji iliyoanza kuibuka mkoani humo na ameahidi kutoa Shilingi Milioni 20 kusaidia ujenzi wa Zahanati ya Somanga.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Aaah,kumbe kama hatutalima wakati mvua inanyesha?poa tu,kama mvua zinanyesha halafu hatulimi kwa kutegemea chakula cha msaada imekula kwetu.Tunalima tuliobahatika kupata mvua ila kwa wenye ukame lazima chakula kipelekwe mzee.God bless Tanzania.

    ReplyDelete

Top Post Ad