Lazaro Nyalandu Alilia Uhuru wa Vyombo vya Habari, Atia Neno ishu ya Nape Kutishiwa Bastola

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mbunge wa Singida Kaskazini (CCM) Lazaro Nyalandu ambaye pia alikuwa Waziri wa Maliasili na Utalii katika serikali ya awamu ya nne, ameguswa na ishu ya kuvamiwa wa kituo cha Clouds Media pamoja na kitendo cha aliyekuwa waziri wa habari Nape kutishiwa bastola ili asiongee na waandishi wa habari muda mchache baada ya kupigwa chini kwenye baraza la mawaziri na nafasi yake kuchukuliwa na Harrison Mwakyembe.


Wabunge wengi wa CCM walikuwa kimya dhidi ya sakata hilo ambapo Ijumaa hii, Nyalandu ametaka matukio hayo kwenda kujadiliwa bungeni.

Kupitia twitter mbunge huyo alitweet,”IMESIKITISHA sana kuona AFISA akimtishia silaha Waziri Mstaafu Nape.Kitendo hicho ni kinyume na maadili ya TAIFA letu na kimedhalilisha NCHI,”

Aliongeza, “Kupitia BUNGE, nitaiomba SERIKALI ichukue HATUA za kinidhamu na kisheria DHIDI ya AFISA aliyemtishia Mh NAPE kwa SILAHA.Kitendo HAKIKUBALIKI,”

Katika sakata la RC Makonda kuvamia kituo cha Clouds Media alitweet, “Katika kutekeleza wajibu wake KIKATIBA, BUNGE ni sharti lijadili na kutoa AZIMIO kuhusu kilichojiri CLOUDS FM, na UHURU wa VYOMBO vya HABARI,”

Pia kitendo hicho kimeweza kupingwa na mashirika mbalimbali habari nchini.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mmmmh sasa hata waliosahaulika watafichuka huko mapangoni arimladi tu wapate airtime au kiki. Wasikike kwamba nao wapo. Mmmh hiii Tanzania ni shidaaa. Lakini tutafika tu kiugumu ugumu na haya magube gube yasiyopenda maendeleo ya Taifa lao, baada ya kuchapa kazi wao wamelalia majungu tu, kwa vile walisha zoea kujizolea vya bila kutolea jasho, wakishilikiana na madrag deler. Washindwe na walegee. Walala ho wamechoka sasa, tena wamewachoka kweli, na kuwajibika familia zao

    ReplyDelete

Top Post Ad