Mahakama Yamnyooshea Kidole Halima Mdee,Yadai Imechoka Kumbembeleza..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemwonya na kumwambia Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema), kwamba kadi za onyo kwa ajili yake zimeisha kutokana na kushindwa kuhudhuria mahakamani siku ya kesi.

Kauli hiyo ilitolewa jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya kubaini kwamba ilitolewa hati ya kumkamata mbunge huyo kwa kushindwa kufika mahakamani.

Halima Mdee alipotakiwa kujitetea aliinuka na kujieleza kuwa amefika mahakamani hapo akiwa na nyaraka za safari ikiwamo tiketi na VISA na kwamba taarifa za safari alimpa wakili.

Kwa upande wa wakili wao, Hekima Mwesiga aliieleza mahakama kuwa nyaraka za kuiarifu mahakama juu ya safari ya Halima Mdee nje ya nchi kwa bahati mbaya hakuziwasilisha, alikuwa nazo Peter Kibatala ambaye alikuwa akiendesha kesi ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.

“Tutaonana wabaya katika hili ni lazima unapofanya kitu adabu yake ifuatwe, Wakili hakufuata taratibu na Halima kabla ya kusafiri ulipaswa kutoa taarifa mahakamani ili uweze kupata ruhusa ya mahakama lakini haukufanya hivyo.

“Sasa nafikiri wote tufuate taratibu za kuhudhuria mahakamani, Halima Mdee kadi zako  za kukuonya zimeisha tafadhali,”alisema Hakimu.

Mdee na wabunge wengine wa Chadema, Mwita  Waitara, Saed Kubenea  na makada wao wanatuhumiwa kumjeruhi Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresa Mmbando.

Kabla ya onyo hilo, mahakama ilisikiliza ushahidi wa upande wa mashtaka uliotolewa na Mrakibu wa Polisi, ambaye pia ni Msaidizi wa Operesheni Ilala, Eugen Mwampondele.

Mwampondele alidai siku ya tukio alimwona Rafii Juma na Halima Mdee wakimkunja Theresa Mmbando ili awape nyaraka.

Shahidi huyo alidai waliompiga Mmbando hawapo mahakamani. Washtakiwa katika kesi hiyo ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea, Diwani wa Kata ya Kimanga, Manase Njema (56), Halima Mdee (37) na Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara (40).

Wengine ni mfanyabiashara na kada wa chama hicho, Rafii Juma (21)pamoja na Diwani wa Kata ya Saranga, Ephreim Kinyafu (33).

Inadiwa kuwa Februari 27, 2016 katika Ukumbi wa Karimjee Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam watu hao walimjeruhi Theresia na kumsababishia majeraha mwilini wakati wa uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad