Maoni ya Zitto Kabwe Kuhusu Uteuzi wa Mama Salma Kikwete na Kuhusu Baa la Njaa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Serikali Ina Kauli Mbili Zinazokingana Juu ya Hali ya Chakula Nchini

Siku nzima ya jaa nilikuwa natakiwa na waandishi wa Habari kutoa maoni yangu kuhusu uteuzi wa Mtanzania mwenzetu, na mke wa Rais aliyepita, Mama Salma Kikwete kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.
Niliwaambia sina maoni yeyote. Leo baada ya magazeti kuandika maoni ya watu mbali mbali nimeulizwa tena. Jibu langu, ambalo ninaliweka hapa kwa umma, ni kwamba Mama Salma Kikwete ana haki zote kama Mtanzania mwengine yeyote kuteuliwa ama kuchaguliwa Kwa mujibu wa Katiba yetu. Hivyo uteuzi wake kwa maoni yangu ni kama teuzi nyengine zozote zile.
Kuolewa kwake na aliyekuwa Rais hakumwondolei yeye haki zake za kikatiba. Kama mwenyewe ataridhia ninamtakia kila la kheri katika kazi yake mpya. Sababu za kuteuliwa kwake anajizuia aliyemteua na baadhi ya wasomi wabobezi Kama Prof. Kitila Mkumbo wamenukuliwa wakifanya uchambuzi mzuri Kabisa kwenye gazeti la The Citizen la Leo.
Kwangu Mimi, kwa maoni yangu, nchi yetu inakabiliwa na mambo makubwa zaidi ya kujadili na kutolea maoni ikiwemo suala la njaa. Serikali kwenye suala hili la njaa imeyumba sana na kwa kiasi flani imewayumbisha pia wananchi wanyonge wanaokabiliwa na tatizo hili, na kwa maoni yangu naamini kabisa Serikali haijatekeleza wajibu inavyostahili. Kama mzalendo kwa taifa langu nachukua wajibu wangu kuonyesha mapungufu hayo ya Serikali pamoja na kutoa njia mbadala.

Jana, Serikali kupitia Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kusisitiza kuwa haitatoa chakula cha msaada kwa Watanzania watakaokabiliwa na njaa. Rais alisema "tumezoea kuambiwa maneno matamu matamu kwamba hakuna mtu atakeyekufa kwa njaa. Mimi nawaambia usipolima utakufa na njaa". Serikali kwa kauli za namna hii inawachanganya watanzania, kwanza ni muhimu sana kujua (na naamini Serikali inajua) kuwa wananchi hawa wamelima, suala la hali ya njaa si kwa sababu ya kutokulima kwao, bali ni kwa sababu kadhaa zilizo nje ya uwezo wao, ikiwemo hali ya hewa yenye mvua chache.
Mfano mikoa ya Singida, Shinyanga
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mnapenda kuchanganya maneno nyie waandishi,
    Rais kasema hivi:kama hatutalima wakati mvua zinanyesha ndio hakuna chakula cha msaada,kwa maanahiyo kwenye mvua watu wasilalamikie njaa,ila kwenye ukame kwa nini asitoe chakula,watakuwa wana sababu ya kukosa mazao tayari,ambayo ni ukame.

    ReplyDelete
  2. Katika viongozi wapinzani huyu jamaa anafaa sana,naona wengi tuanza kuwa na imani nae.

    ReplyDelete
  3. Angry Face... Mimi nimeshakusoma na Nia yako na lengo lako linajulikana.. Sasa Inakuwaje?

    ReplyDelete

Top Post Ad