Mbasha Afichua JPM Alivyomfanyia ya Diamond..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Hii ilikuwa stori lakini haikuandikwa! Mwimbaji wa Nyimbo za Injili Bongo, Emmanuel Mbasha amefichua jambo kwa kueleza kwamba,  aliyemmuingiza yeye pamoja na mtalaka wake, Flora Mbasha katika masuala ya siasa, alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dk John Pombe Magufuli.    

Akizungumza katika mahojiano maalum na Risasi Jumamosi, Mbasha alifunguka kuwa, Rais Magufuli alimpigia simu akiwa studio kama alivyomfanyia staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ hivi karibuni, Clouds TV.

Mbasha alifunguka mambo mengi lakini suala zima la historia yake kisiasa, alisema Rais Magufuli ndiye ilikuwa chachu ya yeye na Flora kujiunga na Chama Tawala, Chama cha Mapinduzi (CCM). “Nakumbuka ilikuwa ni  mwaka 2005, nilikuwa na aliyekuwa  mke wangu, Flora.  Tulienda Clouds FM, wakati huo walikuwa kule Kitega Uchumi, Posta.

Tulikuwa tumeenda kutambulisha wimbo wetu, nakumbuka ulikuwa ni ule Tanzania, sasa baada ya Kipindi cha Gospo Track kuishia,  Mtangazaji George Njogopa alinitaka niseme namba ili wadau waweze kutusaidia.

“Nikataja namba zangu hewani. Sasa kama nusu saa hivi mbele baada ya kipindi kuisha, sisi tulikuwa tunashuka ghorofani, ghafla nikasikia simu inaiita. “Nikapokea, aliyepiga alijitambulisha kwa jina la John.

Akaniambia kuwa hayupo Dar, ila akirudi atanitafuta ili  aweze kunisaidia,” alisema Mbasha.

Mbasha alisema hakuwa na imani kama kweli John atamtafuta tena na hakujua pia alikuwa anataka kumsaidia  kivipi, lakini kama zari, baada ya wiki kupita, alipigiwa simu na kuambiwa aende Posta.

“Yaani sikuamini, John akapiga simu, akatuelekeza twende Posta, nikashangaa  anatuambia tuingie Wizara ya Ujenzi. Tukaingia, akatuambia tumuambie mlinzi  kuwa tunakwenda kwa Waziri Magufuli.

“Moyo wangu ukapiga paah! Nikamuambia Flora,  hakuamini. Tukapanda hadi ghorofa ya pili. Tulipofika, tukakaa kwenye foleni kisha tukaingia na kukutana na Waziri John Magufuli,” alisema Mbasha.

Baada ya macho yao kuamini wamekutana na waziri, Mbasha anasema  aliwakaribisha chai,  wakafanya mazungumzo mafupi na tangu hapo, wakashawishika  kujiunga na CCM, wakawa washiriki shughuli mbalimbali za serikali pamoja na za chama hicho tawala.

“Tangu hapo, mheshimiwa alikuwa karibu sana na sisi. Akawa anatushauri njia nzuri za kupita ili tufanikiwe.

“Nakumbuka tulianza na shughuli ya uzinduzi wa Barabara ya Msamvu.

“ Tukaendelea hivyo  na ikawa kila unaposikia shughuli ya uzinduzi, na sisi lazima tuwepo. Baadaye akatukutanisha na Rais Benjamin Mkapa, kisha Jakaya Kikwete, sisi tukawa kama watoto wa CCM,”alisema Mbasha.

Mwaka 2014, Mbasha na Flora waliachana baada ya Mbasha kudaiwa kumbaka shemejie kisha wanandoa hao kushutuhumiana vikali.

Mbasha alimtuhumu Flora kuhusika na ‘mpango’mchafu ili aweze kumtia hatiani mumewe,  lakini hata hivyo kesi iliunguruma na hatimaye Mbasha aliachiwa huru baada ya upande wa Jamhuri kushindwa kuthibitisha mashtaka
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad